Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Siku mbili zilizopita ilitokea milipuko minne inayoaminika kuwa ni
mabomu katika maeneo matatu tofauti katika visiwa vya Zanzibar na watu
wanne kujeruhiwa.
Akizungumza na Tanzania Daima jana, Mkurugenzi wa kampuni
mmoja ya utalii nchini, Masque Herriton, alisema wamekuwa wakipokea simu
kutoka nchi mbalimbali ambazo zimetaka kujua juu ya hali za wananchi
wao.
“Tuna siku mbili tunapokea simu kutoka mataifa mbalimbali, ambapo
wanahitaji kujua kuhusu wananchi wao walioingia kupitia kampuni yetu
kama wapo salama,” alisema.
Herriton alisema kuna haja ya serikali kuangalia namna ya kupunguza
ama kutokomeza matukio hayo Zanzibar kwa kuwa inaweza kuleta athari
kiuchumi.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment