Mwenyekiti
wa Bodi ya kuchunguza ajali ya Meli ya MV. Kilimanjaro 2, Khamis
Ramadhan Abdallah (katikati) akisoma baadhi ya vipengele vya Ripoti hiyo
wakati wa kumkabidhi Waziri wa Miundo mbinu na Mawasiliano Zanzibar
Rashid Seif Suleiman (Mwenye Kanzu)Ofisini kwake Kisauni nje kidogo ya
mji wa Zanzibar. Picha na Nafisa M. Ali-WMM
Mwenyekiti
wa Bodi ya kuchunguza ajali ya Meli ya MV. Kilimanjaro 2, Khamis
Ramadhan Abdallah (kushoto) akikabidhi Ripoti ya Bodi hiyo baada ya
kukamilika kwa Waziri wa Miundo mbinu na Mawasiliano Rashid Seif
Suleiman Ofisini kwake Kisauni nje kidogo ya mji wa Zanzibar.
Na Nafisa M. Ali –WMM
17/03/2014
Bodi ya
kuchunguza ajali ya Meli ya MV. Kilimanjaro 2 leo imekabidhi rasmi
Ripoti ya ajali hiyo baada ya kumaliza kazi hiyo kwa Waziri wa Miundo
mbinu na Mawasiliano Rashid Seif Suleiman Ofisini kwake Kisauni nje
kidogo ya mji wa Zanzibar. Akikabidhi Ripoti hiyo Mwenyekiti wa Bodi
hiyo Khamis Ramadhan Abdallah amesema kazi hiyo waliyopewa wameweza
kuimaliza kwa mujibu wa siku walizopewa na walikuwa huru bila ya
kuingiliwa na mkono wa Serikali wala Taasisi yoyote.
Aidha
alisema Bodi ilifanya kazi katika mazingira magumu lakini walichukulia
kazi hiyo niyanyumbani na niwajibu wao kufanya kwa Maslahi ya wananchi
wa Zanzibar. Hata hivyo alisema hapo awali kazi hiyo walipangiwa
kuifanya kwa kipindi cha mwezi mmoja lakini kutokana na uzito wa kazi
hiyo na majukumu mengine walilazimika kuomba mwezi mmoja ambapo kazi
hiyo walitakiwa kuikabidhi kesho na badala yake wameweza kuikabidhi leo.
Aidha
mwenyekiti huyo alitoa shukran zake za dhati kwa niaba ya bodi hiyo kwa
mamlaka ya Usafiri Baharini kwa ushirikiano mzuri waliouonesha kwa bodi
hiyo kwa kipindi chote cha kazi hiyo. Kwa upande wake Waziri wa
Miundombinu na Mawasiliano Rashid Seif Suleiman ameipongeza Bodi hiyo
kwa kufanya kazi bila ya upendeleo na zaidi walizingatia uhalisia wa
kazi yao na siyo kubabaishwa na Mtu.
Aidha
alisema chombo hicho hakikuundwa kwa kutafutwa nani mbaya wala mkosa wa
ajali hiyo bali kimeundwa kwa ajili ya kuangalia mapungufu yaliyopo na
kuweza kurekebishwa ili Wazanzibari wasizidi kuumia. Hata
hivyo alisema dalili nzuri ipo katika Ripoti hiyo na kazi iliyobaki ni
kuisoma kwa kina na kisha kukabidhi katika Mikono ya Serikali kuu kwa
mujibu wa taratibu zilizopo. Aidha aliishukuru sana bodi hiyo kwa vile
ilikuwa huru na kuweza kufanya kazi kwa kina bila kizuizi cha mtu wala
Serikali.
Naye
Naibu Katibu mkuu wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Tahir A.K
Abdullah amesema Wananchi hivi sasa wanasubiri kuona Serikali imefanya
nini tokea ajali hiyo imetokea ambapo aliwatoa wasiwasi kuwa haki
itatendeka kwa mujibu wa uchunguzi uliofanyika. Bodi hiyo ya Wajumbe
watano ambayo iliyoundwa chini ya Sheria ya Usafiri wa Baharini kifungu
no. 4552 na 4551 ya mwaka 2006 imeundwa kufuatia ajali ya Meli ya MV.
Kilimanjaro 2 iliyotokea Miezi miwili iliyopita katika Mkondo wa Nungwi
ilipokuwa ikitokea Pemba kuja Unguja.
IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR
0 comments:
Post a Comment