Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Kamishna Mkuu wa Jeshi la Polisi Zanzibar,Mussa Ali Mussa.
Dada huyu (jina linahifadhiwa) aliwaambia waandishi wa habari kwamba badala ya kuiachilia sheria kuchukua mkondo wake, pamekuwapo na juhudi za kumnyamazisha na kumtaka afute kesi kwa kumpa kile kilichoelezwa kama kifuta machozi.
“Nimeahidiwa kupewa Shilingi milioni mbili ili nifunge mdomo, lakini fedha hizi hata kidogo haziwezi kununua utu na heshima yangu,” alisema huku machozi yakimlengalenga kuonyesha jinsi alivyoathirika kisaikolojia.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja, Salma Khamis, alisema ofisi yake imepokea taarifa ya madai ya msichana huyo kufanyiwa kitendo hicho cha ukatili katika hoteli hio ya kitalii na kwamba hivi sasa upelelezi unaendelea.
“Tumeshachukua nguo za huyu dada ambazo zinaweza kusaidia katika upelelezi na tunazifanyia uchunguzi zaidi,” alisema.
Msichana huo ambaye ni mfanyakazi wa kampuni ya ulinzi ya SG Kilimani mjini Unguja, alisema alibakwa akiwa kazini jambo ambalo limemsababishia madhara makubwa.
Alidai kuwa mmoja wa wafanyakazi wa hoteli hiyo alimuomba ampikie chakula katika chumba cha mmoja wa maofisa waandamizi hoteli hiyo na baadaye akambaka.
Baada ya kufanyiwa kitendo hicho cha kinyama aliripoti katika kituo cha polisi cha Kiwengwa ili mtuhumiwa achukuiwe hatua za kisheria, lakini aliachiwa kwa dhamana.
Kiongozi wa kampuni hiyo ya ulinzi, Sadic Katisha, aliliomba Jeshi la polisi kufuatilia kwa kina kesi hiyo ili mtuhumiwa huyo wa ubakaji achukuliwe hatua za kisheria.
Kamishna wa kazi, Kubingwa Mashaka Simba, alisema afisi hiyo haihusiki na matukio ya udhalilishaji kwa wafanyakazi wa mahoteli.
“Mambo ya udhalilishaji ni makosa ya jinai ambayo yanashughulikiwa na jeshi la polisi. Sisi tunashughulikia malalamiko na migogoro ya wafanyakazi” alisema Kubingwa.
SOURCE:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment