Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Kikao cha majadiliano ya Bajeti ya Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar kwa mwaka wa fedha 2014/2015 kitaaza leo katika Baraza la
Wawakilishi kisiwani hapa, miswada miwili ya sheria itawasilishwa na
kujadiliwa.
Hayo yalielezwa na Katibu wa Baraza hilo, Yahya
Khamis Hamad alipozungumza na waandishi wa habari kwa lengo kueleza
shughuli za kikao hicho huko Mbweni nje kidogo ya mji wa Zanzibar.
Hamad aliitaja miswada hiyo kuwa ni ule wa Sheria
ya Fedha pamoja na wa Sheria ya kuidhinisha matumizi ya Serikali kwa
mwaka wa fedha 2014/2015.
Alifafanua kuwa mswada wa fedha ukishapitishwa
ndiyo utakaotoa mwelekeo wa matumizi ya bajeti hiyo kuazia Julai mosi
mwaka huu na kuiruhusu SMZ kutumia kiasi cha fedha kilichoidhinishwa.
“Ni imani yangu kwamba miswada hiyo itapitishwa bila vikwazo ili kuruhusu Serikali kuendesha shughuli zake” alisema katibu huyo.
Pia katibu huyo alieleza mbali na shughuli hizo
katika kikao hicho cha 16 ndani ya baraza la tano, maswali 90 yataulizwa
na kujibiwa.
Alisema kwa mara ya kwanza kikao cha bajeti,
kitaweza kupokea uwasilishwaji wa mpango wa maendeleo ya Zanzibar wakati
wa asubuhi na jioni waziri wa fedha atawasilisha Makadirio na Matumizi
ya Serikali.
Katibu huyo aliwaonya wajumbe wa baraza hilo, wasihusishe Bunge la Katiba na kikao hicho, ili kuepusha malumbano.
Chanzo:Mwananchi
Chanzo:Mwananchi
0 comments:
Post a Comment