Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
KAMPUNI ya mawasiliano Tanzania (TTCL) imeanza ujenzi wa ofisi ya
kisasa ya huduma kwa wateja katika eno la Madungu, Chakechake, Pemba
itakayogharimu sh bilioni 1.2.
Akizungumza na waandishi wa habari visiwani Pemba hivi karibuni kwa
niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Dk. Kamugisha Kazaura, Mkuu wa
Kitengo cha Ufundi, Mtandao na Ukarabati, Jothan Lujara, alisema kampuni
yao inaanza ujenzi katika eneo hilo kama njia ya kujiimarisha katika
utoaji huduma visiwani hapa na nchi nzima kwa ujumla.
“Kwa muda mrefu, tulikuwa tukitoa huduma zetu kwa wateja kwa kutumia
jengo la kukodi katika eneo hili, na sasa tumeamua tuwe na jengo letu,”
alisema.
Alisema kati ya fedha hizo, sh bilioni 1.1 atalipwa mkandarasi
atakayejenga jengo hilo na na sh milioni 93 atalipwa mshauri mwelekezi
wa ujenzi.
“Fedha zote hizi zinagharimiwa na kampuni yetu kutokana na vyanzo
vyake vya mapato,” alisema na kuongeza kuwa jengo hilo litakuwa na
ghorofa moja.
Alisema jengo hilo linatarajiwa kujengwa katika kipindi cha miezi nane na kukamilika Februari mwakani.
Mkuu wa Mkoa Kusini Pemba, Juma Kasim Tindwa, alisema jengo hilo
litasaidia kutoa huduma nzuri Chakechake kwa vile linajengwa kisasa na
lenye nafasi kubwa.
“Leo naikabidhi Kampuni ya MS Quality Building Contractors Ltd ili
ianze rasmi ujenzi huu na matarajio yangu itamaliza kwa wakati,”
alisema.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment