Home » » Vyama vya siasa vyaionya ZEC isipunguze majimbo Zanzibar

Vyama vya siasa vyaionya ZEC isipunguze majimbo Zanzibar

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Tume ya Uchaguzi  Zanzibar (ZEC) imeonywa kuacha mpango wake wa kutaka kupunguza majimbo ya uchaguzi visiwani hapo badala yake wafikirie kuyaongeza au kuyaacha kama yalivyo.

Onyo  hilo lilitolewa na viongozi wa vyama vya sisasa waliohudhuria katika mkutano wa siku moja ulioitishwa na ZEC  mjini Chake Chake

Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima (AFP),  Saidi sodi Said,  alisema inashangaza kuona ZEC inajipanga kupunguza majimbo wakati kumekuwapo engezeko kubwa la watu katika maeneo na mitaa kuongezeka.

Alisema kwa mujibu wa katiba Zanzibar imejiwekea mpango wa kuwa na majimbo 40 hadi 55, hivyo ni vyema tume ikapokea maoni ya kuengeza majimbo na kuachana mpango wa kuyapunguza kupunguza.

“Mimi nilipokuwa mjumbe wa Kamatui ya Mapinduzi nilikuta mwaka 1964 wilya mkoani ina watu 46,648 wakati hivi sasa ina watu 86,0000  marambili y azamani,” alisema Saidi.

Alisema kuwa katika wilaya mkoani kulikuwa na watu 51,000 wakati hivi sasa inawatu 66,000 huku kukiwa na mitaa mingi iliyoongezeka Unguja na Pemba na majimbo yametanuka, hivyo hoja ya kuyapunguza sasa haina mashiko.


 Mjumbe wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Khamis Issa Mohamed, alisema wakati huu ni vyema kuangalia historia hususani mwaka 2005 kutokana na malalamiko yaliyotokea baada ya kupunguzwa majimbo ya Pemba na kuongeza majimbo ya Unguja.

 Alisema kuwa jambo hilo lilisababisha masikitiko na kuonekana kuwa lengo lilikuwa ni kupunguza majimbo ya CUF.

Mwenyekiti waZEC, Jecha Salimu Jecha, alisema ugawaji wa  idadi ya watu mipaka na majimbo ni jambo la kawaida na lipo kwa mujibu wa sheria ya ZEC, na kuomba ushirikiano  wa vyama.

Jecha alisema kazi hio ya kukusanya maoni ya wananchi katika maeneo, vyama vya siasa na asasi za kirai itachukua mwaka moja hadi kumalizika nakwambakazi kubwa inayoikabili ZEC katika kipindi cha miezi sita ijayo ni kuchunguza idadi, majina na mipaka ya majimbo ya uchaguzi Zanzibar.
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

Post a Comment

 
Support by Blogs za Mikoa Tanzania
Copyright © 2012. Zanzibar Yetu - All Rights Reserved
Designed by by Blogs za Miikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa