Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad.
Maalim Seif alisema hayo jana wakati akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika Tandale Kwa Tumbo, ulioandaliwa kwa ajili ya kuwashukuru wanachama wa CUF na wananchi kwa kujipa ushindi chama hicho.
Maalim Seif alisema ni dhahiri matokeo mazuri ya wapinzani yalitokana na uamuzi wa vyama vinne vinavyounda umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kuunganisha nguvu zao na kushindana na CCM, pamoja na kujidhatiti kulinda kura zao zisiibwe.
Alisema CUF pamoja na vyama vinavyounda UKawa kusimama imara kuhakikisha mapandikizi hawaingizwi katika maeneo wasiyohusika, lakini pia walihakikisha wale walioshindwa hawaapishwi kushika nyadhifa hizo.
“Suala la kuendelea na Ukawa halina mjadala kama kweli tunataka tuichimbie kaburi CCM, pale tulipokuwa kila mtu na lake, hatukuwa na nguvu kama tulizonazo sasa,” alisema Maalim Seif.
Katika uchaguzi huo Kata ya Tandale, CUF kilishinda mitaa mitatu kati ya sita, na mtaa mmoja hadi sasa matokeo yake yana utata.
Akizungumza katika mkutano huo, Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Kwatumbo, Mohammed Kassim alisema ushindi huo unatokana na umakini wa wana-CUF kuhakikisha wanadhibiti ujanja wote wa CCM katika hatua zote za uchaguzi.
Hata hivyo aliwataka wanachama wa CUF na wananchi wa Tandale wasiridhike na wasijisahau kwa ushindi huo, lakini wahakikishe wanajiimarisha zaidi na kuhakikisha wote wanajiandikisha katika daftari la kura, ili washiriki katika uchaguzi mkuu wa Oktoba.
CHANZO:
NIPASHE
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment