Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein jana aliungana pamoja na wananchi wa Mkoa
wa Kusini Pemba katika futari maalum aliyowaandalia, ikiwa ni miongoni mwa
utamaduni anaouendeleza wa kufutari pamoja na wananchi wa Mikoa yote ya
Zanzibar kila ufikapo mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Hafla hiyo ya
futari ilifanyika katika viwanja vya Ikulu ndogo ya Chake Pemba, na kuhudhuriwa
na wananchi pamoja na viongozi mbali mbali wa Mkoa huo pamoja na baadhi ya
viongozi wa Serikali.
Aidha, Mama
Mwanamwema Shein naye aliungana pamoja na akina mama wenzake wa Mkoa huo katika
futari hiyo ya pamoja.
Mara baada ya
futari hiyo kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein, Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Hemed Suleiman Abdalla
alitoa shukurani kwa wananchi pamoja na viongozi wote waliohudhuria katik
muwaliko huo.
Kwa aniaba yake,
familia na Serikali, alisisitiza kuendeleza ushirikiano na mshikamano uliopo
kwani ushirikiano ndio nguvu ya kila kitu.
Sheikh Mohammed Suleiman
kutoka Masjid Al-Halil Cheke Chake, akitoa
neno la shukurani kwa niaba ya wananchi hao waliofutarishwa na Alhaj Dk. Shein
alitoa pongezi na shukurani kwa mwaliko huo wa Rais.
Katika shukurani
hizo Sheikh Mohammed alitumia fursa hiyo kueleza furaha waliyokuwa nayo
wananchi hao na kusisitiza kuwa Alhaj
Dk. Shein anapaswa kupongezwa sana kutokana na mengi aliyowafanyia
wananchi wa Zanzibar.
Sheikh Mohammed
alimuelezea Alhaj Dk. Shein jinsi anavyoweza kukaa pamoja na wananchi na kuweza
kushirikiana nao vizuri huku wakitoa shukurani kwa kuiongoza Zanzibar kwa amani
na utulivu hadi leo hii.
0 comments:
Post a Comment