DSC05130Muonekano wa Gari hilo kama linavyoonekana baada ya kupata ajali eneo la kijiji  cha Kibele, Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja Novemba 1, 2015 kwa kile kilichoelezwa kuwa ni mwendo kasi wa gari hiyo.
DSC05127Wananchi wa kijiji  cha Kibele, Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini wakiangalia Gari hilo.
DSC05132
DSC05128Na Mwandishi Wetu.
[Unguja-ZANZIBAR] Mwanajeshi wa  Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (TPDF) imeelezwa kuwa amenusurika katika ajali ya gari iliyotokea mchana  wa leo Novemba Mosi, eneo la kijiji  cha Kibele, Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja kwa kile kilichoelezwa kuwa ni mwendo kasi wa gari hiyo.
Kwa mujibu wa shuhuda wa taarifa ya tukio hilo: “ Ajali imetokea mchana huu kwenye saa 8.10 ambayo imemhusisha askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (TPDF) (jina halikupatikana). Mazingira ya ajali hiyo ambayo imetokea katika kijiji cha Kibele, Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja ni mwendo kasi wa dereva huyo ambaye alishindwa kuidhibiti gari ndogo aina ya Toyota Spacio yenye namba za usajili Z 511 FG na hatimaye kuacha barabara na kugonga  mnazi.
Baada ya kugonga mnazi huo, uliangukia gari na baadae gari kuwaka moto. Dereva alitolewa ndani ya gari akiwa amebanwa na air bags zilizofyatuka na kuokoa uhai wake. Alipata majeraha madogo ya kuchubuka kwenye mikono yake iliyokuwa inavuja damu.
Chanzo: Habari za Jamii Blog