Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Viongozi
wa Kitaifa waliohudhuria mazishi ya Marehemu Mzee Ibrahim Amaan
wakikamilisha hitma ya kumuombea kiongozi huyo Mwanamapinduzi ya
Zanzibar huko Kijijini kwake Nymanzi Wilaya ya Magharibi “B”.
Baadhi
ya waumini wa Dini ya Kiislamu wakisubiri ibada ya sala ya Maiti kwa
ajili ya kumuombea Dua zee Ibrahim Amaan kwenye Msikiti wa Ijumaa
aliokuwa mioingoni mwa watu waliouanzisha Kijijini kwake Nyamanzi.
Waumini
wa Dini ya Kiislamu wakiongozwa na Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh
Hassan Ngwali walimsalia Mzee Ibrahim kwenye msikiti wa Kijiji hicho.
Picha na – OMPR – ZNZ.
MWANAMAPINDUZI
ya Zanzibar ya Mwaka 1964 ambae pia ni mwanzilishi wa Chama cha
Mapinduzi Mzee Ibrahim Aman aliyefariki Dunia jana mchana amezikwa leo
Kijijini kwake Nyamanzi Wilaya ya Magharibi “B” Mkoa wa Mjini Magharibi.
Mzee
Ibrahim aliyekuwa akisumbuliwa na maradhi ya baridi pamoja na Uzee
alilazwa katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja akipatiwa matibabu kutokana
na afya yake.
Mamia
ya Wananchi, waumini wa dini pamoja na Viongozi wa Kitaifa
walihudhuria mazishi hayo yaliyojumuisha pia Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Ali Hassan
Mwinyi pamoja na Makamu wa Rais Mstaafu wa SMT Dr. Mohammed Gharib
Bilal.
Mzee
Ibrahim Amaan alizaliwa mwaka 1930 katika Kijiji cha Nyamazi na
alipofikia umri wa kusoma Wazazi wake wakampelekea kupata elimu ya Quran
iliyoambatana na ile ya Dunia katika ngazi ya Msingi.
Wakati
wa ujana wake marehemu Mzee Ibrahim Amaan alijishughulisha na kazi za
ukulima na uvuvi ili kujipatia kipato kilichomuezesha kuanza kujitegemea
katika maisha yake ya kawaida.
Mwaka
1957 Mzee Ibrahim alijiunga na Chama cha Afro Shirazy Party ambapo
kutokana na uzalendo pamoja na umakini wake alifanikiwa kuwa
muanzilishi wa Umoja wa Vijana wa ASP Mkoa wa Kusini Unguja.
Katika
Uhai wake marehemu Mzee Ibrahim aliwahi kuchaguliwa kuwa Mjumbe wa
Halmashauri ya Chama cha Afro Shirazy Party na kushiriki kuuangusha
Utawala wa kisultani Mwaka 1964 na baadaye kujiunga na Jeshi la Ukombozi
la Unguja akifikia cheo cha Kanal.
Akisoma
Risala ya wakfu wa Marehemu Mzee Ibrahim Makungu Waziri wa Nchi Ofisi
ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dr. Miwinyihaji Makame alisema Chama cha
Mapinduzi, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na ile ya Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania zimepokea kwa masikitiko kifo cha Mwanamapinduzi
huyo aliyejitolea muda wake wa maisha kulitumikia Taifa hili.
Dr.
Mwinyihaji alisema Ushujaa wa Mzee Ibrahim ulimpelekea Rais wa Zanzibar
na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohammed Shein kumtunukia
Nishani ya Ushujaa wa Mapinduzi kwenye sherehe hizo za mwaka 2014.
Alisema
Mzee Ibrahim miongoni mwa majukumu yake kwa Taifa aliwahi pia kuwa
Mbunge wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Katibu wa CCM
Idara ya Umma Afisi kuu ya CCM Kisiwandui pamoja na Mwenyekiti wa kazi
za njia na nnguvu za umeme.
Dr.
Mwinyihaji alifafanua zaidi kwamba Mzee Ibrahim alikuwa Mjumbe wa
Baraza la Wazee la Chama cha Mapinduzi wadhifa ambao aliendelea nao hadi
mauti yalipomfika.
Mzee Ibrahim Amaan aliyezaliwa mwaka 1930 na kufikisha umri wa Miaka 86 ameacha kizuka Mmoja na Watoto Thalathini.
Yarabi aiweke roho ya Marehemu Mzee Ibrahim Amaan mahali pema Peponi amin.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
12/3/2016.
0 comments:
Post a Comment