Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
amemtumia salamu za rambirambi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza
la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein kufuatia kifo cha mmoja
wa wanamapinduzi, Mzee Ibrahim Amani Kilichotokea jana tarehe 11 Machi,
2016 Mjini Unguja.
Mzee
Ibrahim Amani ambaye aliwahi kuwa Waziri na Mjumbe wa baraza la
Mapinduzi Zanzibar, ni mmoja wa Watu 14 waliojitoa muhanga kupambana na
kuuondoa utawala wa kisultani huko Tanzania Zanzibar, na kuondoka kwake
kunafanya idadi ya wanapinduzi waliotangulia mbele za haki kufikia 13.
Katika
Salamu zake, Rais Magufuli amesema kwa mara nyingine Taifa limepoteza
mtu muhimu, Mzalendo wa kweli na ambaye daima alisimama kidete kutetea
Taifa lake dhidi ya vitendo vyenye kuleta madhara.
“Nimeguswa
sana na kifo cha Mzee Ibrahim Amani, maisha yake na nia yake ya
kupigania uhuru na uzalendo kwa taifa lake ni mambo ambayo daima
tutayaenzi” Amesema Rais Magufuli.
Dkt.
Magufuli amemuomba Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein kumfikishia
salamu za pole kwa ndugu, jamaa, marafiki na wote walioguswa na kifo cha
Mzee Ibrahim Amani.
“Tumwombe Mwenyezi Mungu aipumzishe roho ya marehemu Ibrahim Amani mahali pema peponi, Amina.” Amemalizia Rais Magufuli.
Inna lillahi wa inna ilayhi raji’un.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
12 Machi, 2016.
0 comments:
Post a Comment