Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Chama cha wananchi CUF kimeitaka Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar kuhakikisha usalama wa raia na ,ali zao baada
ya kuanza kutokea kwa matukio yanayoashiria uvunjifu wa amani.
Hayo yameelezwa na kaimu mkurugenzi wa
habari na mawasiliano wa chama hicho Bwn Hamad Masoud alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari.
''Katika siku za hivi karibuni, hususan
baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Jecha Salim
Jecha, kutangaza kinyume na katiba ya nchi, kufuta uchaguzi wa 25 Oktoba
2015 na matokeo yake, Zanzibar imeshuhudia uingizwaji na uingiaji
mkubwa wa askari, vifaa na zana nzito za kivita katika visiwa vya Unguja
na Pemba.'' Amesema Bwn Masoud.
''Kuna watu wameanza tayari kuondoka katika
makazi yao kwa kuhofia usalama wao kutoka maeneo ya Pemba na kukimbilia
Mombasa nchini Kenya''-Amesisitiza Masoud
Aidha chama hicho kimevitaka vyombo vya
usalama kutenda haki katika kusimamia amani na mshikamano wa Wazanzibar
na kuacha kupendelea upande mmoja wa wa chama talawa pekee.
Uchaguzi wa Zanzibar unarudiwa tarehe
20.03.2016 baada ya uchaguzi uliopita kufutwa na mwenyekiti wa tume ya
uchaguzi Zanzibar (ZEC) Salum Jecha, kwa madai ya kukumbwa na kasoro za
nyingi ikiwemo ya upinzani kujitangazia matokeo kazi ambayo hufanywa na
Tume ya uchaguzi.
0 comments:
Post a Comment