Na Mwandishi Wetu, Zanzibar.
UMOJA
wa vijana wa Chama cha Mapinduzi(UVCCM) Zanzibar umewataka vijana wa
umoja huo katika Mkoa wa Kaskazini Unguja kuwakumbusha viongozi waliopo
madarakani kwa sasa kutekeleza kwa haraka ahadi walizotoa wakati wa
kuomba ridhaa ya kuingia madarakani katika Uchaguzi Mkuu wa Marudio
uliofanyika mwaka huu.
Umesema
vijana wana haki ya kutumia vikao halali vinavyokubalika katika
utaratibu wa kiuongozi ndani ya UVCCM kuwakumbusha viongozi wa chama
hicho kutekeleza kwa vitendo ahadi walizotoa kwa wananchi wa Zanzibar.
Akizungumza
katika ziara ya UVCCM katika Mkoa huo, Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM
Zanzibar, Abdulghafar Idrissa huko katika ofisi ya jimbo la Jimbo la
Kitope iliyopo Kinduni Unguja.
Alifafanua
kwamba CCM ni chama chenye viongozi makini wanaoahidi na wakatekeleza
hivyo hakuna haja ya vijana kuendelea kulalamika badala yake wafuate
utaratibu kuwakumbusha wahusika watekeleze majukumu yao kwa wananchi.
“
Vijana kumbukeni kuwa kwamba nyie ndiyo mliowaweka madarakani hao
Marais, wabunge, wawakilishi na madiwani hivyo msiwaogope kuwakumbusha
kwa kufuata taratibu wajibu wao wa kutekeleza ahadi zao kwenu na
wakikataa basi rudini kwetu mtwambie na tutayafanyia kazi.”, alisema
Idrissa.
Idrissa
alisisitiza vijana hao kuendelea kuwa wamoja ili waweze kunufaika na
fursa mbali mbali zilizopo katika chama na serikali iliyopo madakani.
Alisema
umoja na mshikamano ndiyo njia pekee itakayowawezesha vijana kubuni
fursa za maendeleo kwa lengo la kujikwamua katika wimbi la umasikini
nchini.
Alisema
vijana ndiyo kundi kubwa katika jamii linalopambana na vikwazo tofauti
katika kusimamia maslahi ya CCM lakini bado wanakabiliwa na changamoto
mbali mbali zikiwemo ukosefu wa ajira,elimu,nyenzo na ukosefu wa kipato
mambo yanayotakiwa kutafutiwa ufumbuzi wa kudumu na mamlaka husika ndani
ya Chama na serikali.
“
Nakuombeni vijana wenzangu tuendelee kuwa wamoja katika kuimarisha na
kusimamia maslahi ya CCM kwani Zanzibar bila ya kuwa na vijana imara na
wazalendo nchi yetu itachelewa kupata maendeleo endelevu.
Pia
vijana tunatakiwa kuwa wabunifu wa kuangalia na kuzitumia fursa
zilizotuzunguka ili kupunguza umasikini unaotukabili katika maisha yetu
ya kila siku.”, alisema Idrissa na kuongeza kwamba UVCCM itaendelea kuwa
daraja la kuwavusha vijana kufikia katika kilele cha maendeleo.
Akizungumzia
changamoto ya ajira, Idrissa alisema suala la ajira katika nchi
zinazoendelea bado ni tatizo kwani hakuna serikali yenye uwezo wa kutoa
ajira kwa wananchi wote bali kinachofanyika ni kufungua milango kwa
Wawekezaji, sekta binafsi pamoja na kuanzisha vikundi vya ujasiria mali
ili viweze kutoa ajira badala ya kutengemea serikali pekee.
Kaimu
Naibu Katibu Mkuu Idrisa, alilitaja lengo la ziara hiyo kuwa ni
kuwashukru wananchi wa Zanzibar hasa makundi ya vijana walioshiriki
katika mazingira tofauti kuiweka madarani serikali ya CCM inayoongozwa
na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohamed
Shein.
Alisema
kwamba ushindi wa CCM uliopatikana katika Uchaguzi Mkuu wa Marudio
uliopatikana katika Machi 20, mwaka huu na kupata ushindi wa zaidi ya
asilimia 91 dhidi vya vyama vya upinzani vilivyoshiriki katika uchaguzi
huo.
Alifafanua
ushindi wa chama hicho umetokana na ukongwe wa Demokrasia iliyoimarika
ndani na nje ya chama hicho katika utekelezaji mzuri wa Ilani ya
Uchaguzi kwa vitendo kwa wananchi wote.
Alisema baada ya kumalizika uchaguzi mkuu kilichobaki ni kuimarisha chama hicho ili kiendelee kuwatumikia wananchi kwa vitendo.
Nao
vijana wa umoja huo kwa nyakati tofauti wameahidi kuifanyia kazi
miongozo waliyopewa katika hafla hiyo na kusema kwamba wataendelea kuwa
waumini wa kweli wa CCM kwani ndiyo chama pekee kinachojali maslahi
mapana ya vijana.
0 comments:
Post a Comment