Na Mwandishi Wetu, Zanzibar.
BAADHI
ya Wananchi wa Shehia ya Mwera Kikokani Wilaya ya Magharibi “A” Unguja
wameiomba serikali kuwatembelea wahanga wa mafuriko wa maeneo hayo ili
kufahamu changamoto zinazowakabili kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu,
kabla hawajapata maafa makubwa.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti wananchi hao wamedai kuwa toka wamepata mafuriko
takriban wiki mbili zilizopita hakuna kiongozi yeyote wa serikali
aliyeweza kufika katika eneo hilo kwa kuwafariji ama kutoa msaada wowote
wa kibinadamu.
Akizungumza
mmoja wa wakaazi wa eneo hilo, Kadika Khamis alisema kuwa yeye ni
miongoni mwa wananchi waliokumbwa na mafuriko hayo na kuhama nyumba yake
baada ya kujaa maji ambapo kwa sasa ameomba hifadhi kwa jamaa zake.
Khamis
alisema chanzo cha Mafuriko hayo ni kutokana na mvua kubwa zilizonyesha
na kujaza maji katika bonde la Mtofaani ambayo njia yake imezibwa na
ujenzi wa barabara pamoja ujenzi holela na kusababisha maji hayo kuingia
katika makaazi ya watu.
“Maeneo
haya siyo sehemu ya mabonde na hayajawahi kujaa maji wala kutokea
mafuriko wakati wa msimu wa mvua, hivyo hii ni mara ya mwanzo lakini
imesababisha hasara kubwa kwani mpaka sasa tumehama makaazi yetu na
hatujui matatizpo haya yataisha lini kwani mpasa sasda babo maji yapo
katika majumba yetu kama mnavyoyaona.”, alisema Khamis.
Kwa
upande wake, Rajab Simai alisikitishwa na kitendo cha viongozi wa
serikali hasa viongozi wa jimbo kushindwa kuwatembelea wananchi hao
ambao kwa sasa wanaishi katika mazingira magumu.
Alisema
kwamba kutokana na mafuriko hayo kwa sasa wananchi hawana huduma muhimu
za kibinadamu zikiwemo malazi, chakula na maji safi kwani vyote
vimeangamizwa na maafa hayo.
“
Tunawaomba serikali kuu waje wafanye japo ziara huku na kutuona maisha
tunayoishi kwani watu wamehama katika nyumba zao wengine zimeanguka, na
tunaishi maisha magumu tunahitaji msaada.”alisisitiza Simai.
Simai
alieleza kwamba kutokana na maji yaliyotwaama katika maeneo hayo ambayo
ni makaazi ya watu na kusababisha uharibifu wa miundombinu ya maji safi
kuna hatari ya wananchi kupata maradhi ya kipindupindu kwani maji
wanayotumia kwa sasa siyo salama na hayafai kwa matumizi ya binadamu.
Akizungumzia
hali hiyo Balozi wa nyumba kumi, Sharifa Hassan Ali alikiri kuwepo kwa
uharibifu wa makaazi ya wananchi uliosababishwa na mvua za mafuriko
zilizonyesha siku kadhaa zilizopita.
Alisema
kwamba baada ya kutokea hali hiyo alipeleka taarifa kwa Sheha wa Shehia
ya Mwera ili aweze kukagua na kuhesabu nyumba zilizoathirika na
kupeleka taarifa hiyo kwa ngazi za juu serikali lakini hawakupata
mrejesho wowote mpaka sasa.
Sharifa
alisema kwamba kutokana na hali iliyopo katika eneo hilo kuna baadhi ya
wananchi wanatumia muda mwingi kuwachunga watoto wao wasiende kuchezea
maji machafu yaliyotwaama katika eneo hilo ili wasipate maradhi ya
kipindupindu.
Kwa
upande wake Sheha wa Shehia hiyo, Khamis Bilal Risasi alikiri kuwepo
kwa tatizo hilo na kufafanua kwamba yeye baada ya kupata taarifa za
maafa hayo alienda kukagua na kuwafariji wananchi waliopata maafa hayo.
Alipoulizwa
suala la kutotoa ushirikiano kwa wahanga wa mafuriko hayo, alikanusha
na kueleza kwamba yeye ni miongoni mwa viongozi wa serikali walioenda
kukagua sehemu ya tukio hilo.
“
Hao wananchi wanaosema kwamba eti hakuna kiongozi yeyote aliyefika
katika eneo hilo kuwafariji sio kweli mimi pamoja na mwakilishi wa jimbo
letu tulienda kuwakagua na tukawataka waliokuwa hawana sehemu za kuishi
tuwatengenezee kambi huko Beit-el-sie wakakataa”. Alieleza Sheha huyo
licha ya kutoweka wazi kama taarifa hizo alizifikisha Idara ya Maafa
Zanzibar au la.
Alisema
kuwa robo tatu ya eneo la shehia ya Mwera limezungukwa na mito ya maji
pia kuna baadhi ya wananchi wanaoishi maeneo ya juu wamejenga katika
miundombinu ya kusafirisha maji ya mvua hivyo mvua zikinyesha nyingi
maji hayo yanakosa njia za kupita na kupelekea kuvamia makaazi ya
wananchi wasiokuwa na hatia.
Aidha
alipoulizwa suala la kuwepo kwa huduma za dawa za kutibu maji(water
gurd) na vyandarua vya kuwagawia wananchi, alisema kuwa aliwahi kupewa
vidonge 300 ambavyo havikukidhi mahitaji kwani aliwagawia baadhi ya
wananchi waliopo katika mazingira hatari ya kupata kipindupindi na mgao wa vyandarua alisema shehia hiyo haijapata.
Akizungumzia
maradhi ya kipindupindu Sheha Risasi aliwasihi wananchi wa maeneo hayo
kuweka mazingira yao katika hali ya usafi kwa kutumia vyoo vilivyokuwa
katika sehemu salama pamoja na kuchemsha maji kabla ya kuyatumia ama
kunywa ili kujikinga na maradhi ya miripuko hasa kipindupindu.
Zaidi
ya Nyumba zinazokadiliwa kufikia 70 zimekubwa na mafuriko hayo na kati
ya hizo nyumba 40 wakaazi wake wamehama kutokana na maji kuingia ndani
ya nyumba hizo na kuharibu mali na miundombinu mbali mbali zilizokuwemo
katika nyumba hizo.
0 comments:
Post a Comment