Na Mwandishi Wetu, Zanzibar.
UMOJA
wa vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Zanzibar umewaagiza Makatibu
wa umoja huo katika Mkoa wa Kusini Unguja kusimamia mchakato wa
kuanzisha vikundi vya Ujasiria Mali ili Vijana wapate fursa za
kujiajiri.
Agizo
hilo limetolewa na Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa Umoja huo Zanzibar,
Abdulghafar Idrissa katika ziara Maalum iliyofanyika Mkoa wa Kusini
Unguja ya kuwashukru wafuasi wa CCM na wananchi kwa ujumla waliokipa
nafasi ya kurudi madarakani Chama cha Mapinduzi katika Uchaguzi Mkuu wa
Marudio Zanzibar.
Amesema
njia pekee ya kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa ajira nchini ni
lazima kuwepo na mipango mbadala ya kubuni fursa za ajira kutoka katika
mazingira yaliyowazunguka kwa kuanzisha vikundi vya ujasiriamali ili
vijana waweze kujiajiri wenyewe.
Abdulghafar
ameeleza kwamba makatibu wa umoja huo wanatakiwa kusimamia ipasavyo
mchakato wa kuanzisha vikundi mbali mbali vya ujasiriamali
vitakavyowaunganisha vijana wa UVCCM katika jukwaa moja ili waweze
kupata fursa za mikopo kwa urahisi kutoka serikalini itakayosaidia
vikundi hivyo.
Kaimu
Naibu Katibu Mkuu huyo, amefafanua kwamba tatizo la ajira ni changamoto
ya kidunia sio Zanzibar pekee kwani serikali ina uwezo wa kuajiri
wananchi 27,000 wakati idadi ya watu wote inakadiliwa wastani wa
wananchi milioni 1.5, hivyo nafasi za ajira ni chache hali inayotakiwa
wananchi kutafuta fursa nyingine za kujiajiri wenyewe.
Akizungumzia
lengo la ziara hiyo amesema UVCCM inawashukuru wananchi wote hasa
waliokiamini na kukipa ridhaa Chama cha Mapinduzi Zanzibar katika
uchaguzi mkuu wa Marudio na kupata kikapata ushindi wa zaidi ya
asilimia 91.
Amesema
ushindi huo umetokana na nia ya dhati ya wananchi walioichagua CCM
kutokana na utekelezaji wake mzuri wa Ilani za Uchaguzi za chama hicho
katika Nyanja za kiuchumi, kijamii na kisiasa.
Amesema
CCM bado ina mikakati ya muda mrefu ya kuhakikisha kila mwananchi
anapata maisha bora yanayoendana na kasi ya ukuaji wa uchumi wa nchi.
Ziara
hiyo inaendelea katika Zanzibar nzima kwa upande wa Unguja na Pemba
kwa lengo la kuwashukru na kukutana na wananchi wote na makundi ya
vijana walioshiriki katika zoezi la Uchaguzi Mkuu wa Marudio.
0 comments:
Post a Comment