Na Is-haka Omar, Zanzibar.
CHAMA
cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, kimewashukru na kuwapongeza Viongozi na
wanachama wa Chama hicho walioshiriki na kufanikisha ziara ya Makamo
Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein iliyofikia kilele
chake jana.
Akitoa pongezi hizo kupitia taarifa kwa vyombo vya Habari, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar huko Afisini Kuu ya Chama Kisiwa ndui Mjini hapa, alisema ziara hiyo imekuwa na mafanikio makubwa kwa maendeleo ya CCM na nchi kwa ujumla.
Alisema
kupitia ziara hiyo CCM imeweza kuongeza ari na hamasa kubwa kwa
viongozo, watendaji na wafuasi wa Chama hicho ikiwa ni sehemu ya
maandalizi ya kujipanga na uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka 2020.
Vuai
alifafanua kwamba Chama hicho kina azna na rasilimali kubwa ya wananchi
hasa wafuasi wa CCM wanaokiamini na kukipa ridhaa ya kushinda kwa
kishindo kwa kila uchaguzi mkuu kutokana na utekelezaji wa Ilani za
Uchaguzi za Chama hicho.
Alieleza kwamba pongezi hizo ni maalum kwa viongozi
wa CCM wakiwemo Mabalozi wa Mashina, Wenyeviti na Makatibu wa Matawi,
Maskani, vinaja na Wazee waliojitokeza katika vikao vya Makamo
mwenyekiti huyo kwa upande wa Mikoa yote Kichama Zanzibar.
Wengine
ni watendaji wa CCM Afisi Kuu Zanzibar, Viongozi wa Chama na Serikali
waliofuatana na Dkt. Shein katika ziara zake kichama zilizofanyika
nchini.
Alisema
lengo la ziara hiyo ni kuwapongeza viongozi hao na wafuasi wa CCM kwa
ujumla walioshiriki katika Uchaguzi Mkuu wa Marudio uliofanyika Machi 20
mwaka huu pamoja na kuimarisha Chama.
“
Nawapongeza Viongozi wote walioshirikiana nasi katika ziara ya Makamo
Mwenyekiti wetu Dkt. Shein, hakika mmetujengea imani na kutupa nguvu za
kuendelea kusimamia maslahi ya chama chetu popote bila ya hofu.
Pia
tumejifunza na kupata mambo mengi zikiwemo Changamoto na Mafanikio
yaliyofanywa na CCM pamoja na Chama kwa muda mfupi toka serikali ya Dkt.
Shein kuingia mdarakani.”, Alisema Vuai na kuongeza kuwa CCM ni chama
cha watu wote wa rika na makundi tofauti na kitaendelea kulinda na
kusimamia amani huku kikipinga vitendo vya ubaguzi na kuwagawa wananchi
kwa itikadi zao.
Sambamba
na Hayo aliwapongeza watu wote walioshiriki kwa namna moja ama nyingine
katika maandalizi ya ziara hiyo kuanzia mwano hadi kufikia kilele.
Katika ziara hiyo Dkt.Shein alipata fursa ya kuzungumza na Viongozi hao wakiwemo Mabalozi, Wenyeviti na Makatibu wa Matawi wapatao 16,000 wa Wilaya 12 na Mikoa Sita (6) Kichama Unguja na Pemba.
0 comments:
Post a Comment