Na Masanja Mabula –Pemba
SERIKALI
ya Mkoa wa Kaskazini Pemba imeelezea kusiitishwa na matendo ya hujuma
yanavyoendelea kutokea katika Mkoa huo ambapo kwa sasa imejipanga
kuidhibiti hali hiyo kwa nguvu zote ili isiendelea kuleta athari zaidi
kwa wananchi .
Hayo
yamebinishwa na Mkuu wa Mkoa huo Omar Khamis Othman katika kikao cha
Pamoja kati ya Vikosi vya Ulinzi na Usalama , Maafisa wadhamini wa
Wizara pamoja na wakuu wa Wilaya pamoja na watendaji kutoka Halmashauri
na Baraza la Mji Wete katika Ukumbi wa Jamhuri Wete .
Amesema
uvumilivu na ustahamilivu uliofaywa na Serikali dhidi ya matendo hayo
licha ya kutoa taaluma ya kuachana na matendo hayo kupitia viongozi wa
dini , wanasiasa na watu maarufu lakini imeonekana kwamba vitendo hivyo
vinazidi kushamiri siku hadi siku kwa kuhujumu mali na kutishia usalama
wa wananchi jambo ambalo kwa sasa halikubaliki tena.
Aidha
ameelezea kusikitikishwa na maafia wadhamini kushindwa kuyakemea
matukio hayo licha ya kwamba yanagusa wizara wanazoziongoza huku
akibainisha kwamba baadhi ya watendaji katika wizara hizo wanatumika
kufanya ushawishi wa matendo hayo katika vijiji wanavyoishi .
“Imefika
wakati serikali kuchukua hatua stahiki juu ya wahusika wa matendo hayo ,
kwani inashangaza kwamba tangu yaanze kutokea hakuna Afisa mdhamini
aliyeweza kukemea na imaaminika baadhi ya wafanyakazi wenu wanatumika
kufanya ushawishi ili yaendelee kutokea ”alisema .
Hata
hivyo Afisa Mdhamini Wizara ya Kilimo ,Maliasili , Mifugo na Uvuvi
ameanza kufanya tathmini na mali na mazao yaliyoharibiwa pamoja na
kuwapa misaada ya mbegu na mbolea kwa wakulima waliopata kuharibiwa
mazao yao ili kujiimarisha za shughuli zao za kilimo .
Alisema
wakulima waliopatiwa msaada ni wale wa mpunga , mihogo , viazi na
migomba wakati walioharibiwa mikarafuu na minazi wanasubiri mpaka kuanza
kwa msimu wa mvua za masika ili wawape miche .
“Tayari
sisi Wizara tumewafanyia tathmini wakulima walioharibiwa mazao yao ,
ambapo wengine tumewapa mbegu na mbolea lakini wananchi walioharibiwa
mikarafuu na minazi ambao wao tutawapa miche wakati wa mvua za masika
kuanza ”alieleza.
Hata
hivyo Kaimu kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba Issa Suleiman
Juma aliwataka watendaji wa Wizara ya Kilimo kuharakisha kutoa tathmini
na thamani ya mali zilizo haribiwa ili wahusika wafikishwe kwenye vyombo
vya sheria.
Alisema
, mbali na kuharakisha kutoa tathmini pia aliwataka kuwa tayari kwenda
kutoa ushahidi unapohitajika jambo ambalo litasaidia wahusika kutiwa
hatiani na kukomesha matendo hayo .
0 comments:
Post a Comment