Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
NA HAJI NASSOR, PEMBA
TIMU mpya wa madaktari nane (8)
kutoka China waliopo hospitali ya Mkoa ya Abdalla Mzee Mkoani Pemba, imesema
mpango wa kuwafuata wanafunzi wadogo na kuwafanyia vipimo vya kiafya, utakuwa
endelevu kila baada ya muda.
Kauli hiyo imetolewa na kiongozi mkuu wa madaktari hao
Chen Er Dong, alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi hospitali hapo,
mara baada ya kuamalizika kwa zoezi la vipimo walilolifanya kwa wanafunzi wa
skuli ya msingi ya Makombeni wilaya ya Mkoani hivi karibuni.
Alisema
timu hiyo ya madaktari inataka kuwa na kitu cha aina yake cha kuwafuata
wanafunzi popote waliopo kisiwani Pemba, ili kuwafanyia vipimo vya masikio, pua
na koo ‘ENT’ na kuwapa elimu ya kujikunga na magonjwa yatokanayo na viungo
hivyo na kishaa kuwapa dawa.
Dk
Chen alisema, kwa kuanzia wameanza na skuli hiyo ya Makombeni, ingawa kila
baada ya muda wanatarajia kuwafikia wanafunzi wa skuli nyengine, ili kuwapa
elimu na kisha kuwafanyia vipimo.
“Wanafunzi
wanaonekana wananyemewa na michubuko au athari ya masikio, pua na koo maana
wanaruhusu viungo hivyo kuingia vumbi’’,alisema.
Hata
hivyo alisema kwenye zoezi hilo walilolifanya na madaktari wenzake, hawagundua
mwanafunzi alieathirika sana ingawa wanaonekana kunyemelewa.
Katika
hatua nyengine kiongozi huyo wa madaktari kutoka China, amewataka wazazi na
walezi kujenga utamaduni wa kuwafikisha hospitali watoto wao, ili kufanyiwa
uchuguzi hata kama hawajaanza kuugua.
Kwa
upande wake msaidizi madaktari hao kutoka China dk He, alisema wananchi wa
kisiwa cha Pemba, wasisite kuitumia hospitali Mkoa iliopo Mkoani, ambayo kwa
sasa ina dawa na vifaa mbali mbali vya kisasa.
“Hopsitali
ya Mkoani baada ya serikali ya watu wa China kwa kushirikiana na Serikali ya Zanzibar,
wa meshaiimarisha kila hali, sasa ni wajibu wa wananchi kuitumia’’,alishauri dk
He.
Mwalimu
mkuu wa skuli hiyo ya Msingi ya Makombeni Othman Machano Mmanga, alisema ujio
wa madaktari hao kwenye skuli hiyo, kumeibua mambo kadhaa ya kiafya hasa baada
ya kuwapa elimu.
“Mimi
napendekeza kama ingekuwa inawezekana kila mwaka waje mara tatu, maana ni jambo
jema lenye kuhusiana na afya za wanafunzi ambao hawana utamaduni wa kuchunguuza
afya zao’’,alifafanua.
Hata
hivyo mwalimu Mkuu huyo, amewaomba madaktari hao kwenda na skuli nyengine kwa
ajili ya zoezi la kuchunguuza afya za wanafunzi, hasa kwa vile jamii haina
utamaduni wa kuchunguuza afya zao kama wakijihisi ni wazima.
Timu
hiyo ya madaktari wapya kutoka China, waliwasili mwezi mmoja uliopita kisiwani Pemba,
baada ya wenzao waliokuwepo kumaliza muda wao, kwenye hospitali hiyo ya ya mkoa
ya Abdalla Mzee Mkoani Pemba.
0 comments:
Post a Comment