Imeandikwa na Khatib Suleiman, Zanzibar
SERIKALI ya Mkoa wa Kaskazini Pemba imepiga marufuku watoto chini ya
umri wa miaka 18, kuhusishwa na uvunaji wa karafuu katika kipindi cha
msimu wa mavuno kilichoanza sasa.
Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Omar Khamis Othman alisema hayo
katika uzinduzi wa msimu wa mavuno ya karafuu na kusema imebainika wapo
baadhi ya wazazi kuwahusisha watoto katika kazi za uvunaji wa karafuu,
kitendo ambacho ni kinyume na sheria za nchi na mikataba ya kimataifa.
Alisema katika msimu wa mavuno ya karafuu katika kipindi cha miaka
miwili, baadhi ya watoto waliohusiswa na kazi za uchumaji wa karafuu
walianguka na kupata madhara makubwa.
Aidha Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mwanajuma Majid Abdalla alisema
tayari wametoa matangazo yanayokataza wazazi kuwashirikisha watoto chini
ya umri wa miaka 18 kujishughulisha na kazi za uchumaji wa karafuu.
Alisema madhara makubwa yamepatikana kwa watoto waliohusishwa na kazi
za uchumaji wa karafuu ambapo wapo waliopata ulemavu wa kudumu baada ya
kuanguka wakati wakichuma karafuu.
“Tumetoa matangazo yanayokataza kabisa jamii kuwahusisha watoto chini
ya umri wa miaka 18 na kazi za uchumaji wa karafuu kwa sababu ni kwenda
kinyume na sheria za nchi za kuwashirikisha watoto katika ajira ngumu,”
alisema.
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Taifa la Biashara (ZSTC), Seif
Mzee ambao ndio wanunuzi pekee wa zao la karafuu, wamesema hawatahusika
na malipo ya fidia kwa mtoto chini ya miaka 18 aliyeanguka wakati
akichuma karafuu kwa sababu ni kinyume na sheria za nchi. Alisema
kitendo cha kulipa fidia kwa watoto walionguka katika mikarafuu ni sawa
na kuhamasisha ajira za watoto ambazo zimepigw
CHANZO HABARI LEO
0 comments:
Post a Comment