Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Moja
ya gari lililobeba mchele ulioharibika likishushwa na Wafanyakazi wa
Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar katika Dampo la Kibele Mkoa
Kusini Unguja.
Gari
la kijiko kutoka Wizara ya Ujenzi na Mawasiliano likiangamiza mchele
tani 27.5 ulioharibika katika Dampo la Kibele Mkoa Kusini Ungua.
Picha na Makame Mshenga.
Na Ramadhani Ali – Maelezo
Wafanyabiashara
wa Zanzibar wanaoagiza bidhaa kutoka nje wametakiwa kuwa waadilifu na
kuwahurumia wananchi wenzao wakati wanaponunua bidhaa kwa kuangali ubora
na kuacha tabia ya kuchukua bidhaa dhaifu zenye bei ndogo kwa lengo la
kutafuta faida kubwa.
Mkuu
wa Kitengo cha ufuatiliaji madhara ya chakula kutoka Bodi ya Madawa na
Vipondozi Zanzibar Bibi Aisha Suleiman alitoa ushauri huo wakati bodi
hiyo ilipofanya zoezi la kuangamiza tani 27.5 za mchele ulioharibika na
chakula mchanganyiko kilo 400 kilichomaliza muda ikiwemo tende na juice
katika Dampo la Kibele Mkoa Kusini Unguj.
Bi.
Amina ambae alikuwa msimamizi mkuu katika zoezi hilo alisema mchele
ulioharibika uliingizwa nchini na Kampuni ya Zenj General Machandise na
uliingia maji wakati wa kusafirishwa na chakula kilichomaliza muda wa
matumizi kiligundulika katika maduka mbali mbali ya Zanzibar baada ya
kufanyika ukaguzi katika maduka hayo.
Alisema
kwa mujibu wa sheria bidhaa zinapoharibika wakati wa kusafirishwa na
ikagundulika wakati wa ukaguzi bandarini kabla ya kuingia sokoni mmiliki
wa bidhaa hiyo huwa hanakosa na hulazimika kutoa gharama za kuangamiza
bidhaa hiyo yeye mwenyewe.
Alisema
Kampuni ya Zenj General Machandise ilikubali kutoa gharama ya
kuangamiza mchele huo na kazi hiyo imefanyika chini ya usimamizi wa Bodi
ya Chakula Dawa na Vipodozi.
Alikumbusha
kwamba wananchi wanapotumia chakula kibovu kilichopitwa na wakati
wanapata madhara makubwa ikiwemo maradhi hatari ya kensa ambayo matibabu
yake yanagharama kubwa na yanapoteza maisha ya wananchi wengi.
Ameongeza
kuwa athari ya kutumia chakula kibovu inaweza kuonekana katika kipindi
kifupi tu baada ya kula lakini athari nyengine inaweza kuchukua miaka
mingi kugundulika.
Hata
hivyo amewashauri wananchi kwa upande wao kuwa waangalifu wakati wa
kununua bidhaa za chakula na kuhakikisha kuwa bidhaa wanazochukua
zinakuwa salama kwa matumizi ya binadamu.
0 comments:
Post a Comment