Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ally Iddy akihutubia wakati wa kufunga Kongamano la nne la Watanzania waishio ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) katika hafla
ya chakula cha jioni iliyojulikana kama Swahili Barbeque Night
iliyofanyika mji Mkongwe katika ukumbi wa Ngome kongwe-Zanzibara. (Picha
zote na Mathias Canal)
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Ikulu Mhe Issa Haji Gavu akitoa salamu kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufunga Kongamano la nne la Watanzania waishio ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) katika hafla
ya chakula cha jioni iliyojulikana kama Swahili Barbeque Night
iliyofanyika mji Mkongwe katika ukumbi wa Ngome kongwe-Zanzibara.
Washiriki wa Kongamano la nne la Watanzania waishio ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) wakifatilia hotuba ya Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ally Iddy katika hafla
ya chakula cha jioni iliyojulikana kama Swahili Barbeque Night
iliyofanyika mji Mkongwe katika ukumbi wa Ngome kongwe-Zanzibara.
Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ally Iddy (Kushoto) akifatilia burudani mbalimbali wakati wa kufunga Kongamano la nne la Watanzania waishio ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) katika hafla
ya chakula cha jioni iliyojulikana kama Swahili Barbeque Night
iliyofanyika mji Mkongwe katika ukumbi wa Ngome kongwe-Zanzibara,
Mwingine ni Balozi Anisa Mbega Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora Wizara ya
Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ally Iddy akihutubia wakati wa kufunga Kongamano la nne la Watanzania waishio ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) katika hafla
ya chakula cha jioni iliyojulikana kama Swahili Barbeque Night
iliyofanyika mji Mkongwe katika ukumbi wa Ngome kongwe-Zanzibara.
TAZAMA PICHA ZAIDI
Na Mathias Canal, Zanzibar
Kongamano
lilodumu kwa siku mbili kwa kuwakutanisha watanzania waishio Ughaibuni
(4th Tanzania Diaspora Conference) limehitimishwa hii leo Agosti 24,
2017 huku likiwa limehudhuriwa na Diaspora 350 na kuchagizwa na
wahudhuriaji wengine ambao ni watendaji kutoka taasisi za serikali na
wadau katika uwekezaji na uchumi.
Kongamano
la nne la Watanzania waishio ughaibuni (4th Tanzania Diaspora
Conference) lilifunguliwa jana tarehe 4 Agosti 2017 na Waziri wa nchi
Ofisi ya Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania
anayeshughulikia Mazingira Mhe Januari Makamba (MB) alipomuwakilisha
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia suluhu
Hassan ambapo limefikia ukomo kwa kupatikana majibu ya changamoto
mbalimbali ziwahusuzo Diaspora ikiwemo uraia pacha na sera ya utambuzi
wao nchini Tanzania.
Akihutubia
mamia ya watanzania walioshiriki katika hafla ya chakula cha jioni
iliyojulikana kama Swahili Barbeque Night iliyofanyika mji Mkongwe
katika ukumbi wa Ngome kongwe-Zanzibara, Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ally Idd alisema
kuwa serikali inawatambua Diaspora kama mabalozi muhimu katika
kutangaza utalii Duniani kote jambo ambalo kwa kiasi kikubwa linaongeza
kipato cha nchi.
Alisema
kuwa serikali inatambua kazi kubwa inayofanywa na Diaspora katika
kuitangaza nchi ya Tanzania na vivutio vyake hivyo kuwataka kutumia
fursa hiyo pia kuwatangaza viongozi wa serikali kwa weledi mpana pasipo
kueneza chuki dhidi ya viongozi wao.
Mhe alozi Seif alisema
kuwa kumekuwa na watanzania waishio nje ya nchi wasiokuwa na weledi na
nidhamu dhidi ya viongozi wa serikali kwani wamekuwa wakiwasema vibaya
kwa kuwatukana na kejeli jambo ambalo linarudisha nyuma heshima yao
waliyonayo na kutia doa serikali.
Alisema
kuwa Diaspora wanapaswa kuendelea kushiriki katika makongamano mengine
yajayo kwani kufanya hivyoi kunatoa fursa kwao kuishauri serikali na
kuona namna bora ya utambuzi wao.
Alisema
serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi ili Diaspora waweze
kutumia fursa ya uwekezaji nchini kwa urahisi huku akiwasihi kutumia
fursa muhimu za uwekezaji katika Nyanja zote kwani faida itakuwa kwa
Diaspora wenyewe, watanzania waishio nchini na Taifa kwa ujumla wake.
Alisema
kuwa ushirikiano huo wa Diaspora kupitia makongamano yote yaliyopita
umeimarisha zaidi mahusiano chanya bila kujali dini wala kabila jambo
ambalo limeongeza utu, umoja na mshikamano.
Mhe
alozi Seif alisema kuwa Diaspora wanatakiwa kuheshimu sheria, taratibu
na taratibu za nchi wanazoishi ili kue delea kuipatia sifa chanya
serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
“Naomba
nikukumbusheni nyote mliohudhuria hapa hii leo kutamnbua kuwa mchumia
juani hulia kivulini nanyi kivulini kwenu ni hapa nyumbani hivyo tumie
fursa ya uwekezaji vizuri huku mkikumbuka kuwa mkataa kwao ni mtumwa
zaidi endelezeni umoja na mshikamano kwani inafahamika kuwa umoja ni
nguvu na utengano ni udhaifu.” Alisema Balozi Seif Ally Idd
Kongamano la nne la watanzania waishio ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) linaratibiwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kusudio la kuwaweka pamoja watanzania hao ili kujadili kwa pamoja namna ya kutumia fursa za uwekezaji.
Kongamano la nne la watanzania waishio ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) linaratibiwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kusudio la kuwaweka pamoja watanzania hao ili kujadili kwa pamoja namna ya kutumia fursa za uwekezaji.
Kongamano
kama hilo linaakisi makongamano matatu ya utangulizi yaliyofanyika
mwaka 2014 na 2015 Jijini Dar es Salam huku kongamano la mwaka 2016 na
mwaka huu 2017 yakifanyika visiwani Zanzibar huku likiwa limebebwa na
dhamira ya “Uzalendo kwa Maendeleo” chini ya kauli mbiu isemayo “Mtu Kwao, Ndio Ngao”
Kongamano
la watanzania waishio ughaibuni kwa mwaka 2017 limedhaminiwa na PBZ
Bank, ZSSF, Idara ya Uhamiaji, Sea Cliff Hotel, CRDB Bank, Mult Colour,
Equity Bank, Zanzibar Cable Television, ZBS, Watumishi Housing
Cooparation na Petro.
0 comments:
Post a Comment