Na Is-haka Omar, Zanzibar.
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed
Shein ameutaka Uongozi wa Mkoa wa Kusini Unguja kutangaza na kuelimisha
wananchi juu ya umuhimu wa kuenzi dhana ya Utalii wa ndani.
Kauli
hiyo aliitoa katika majumuisho ya ziara ya Mkoa huo iliyofanyika katika
ukumbi wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA), alisema dhana ya utalii
wa ndani ni muhimu kuendelea kutangawa kwani imebeba fursa
zitakazoongeza pato la taifa kupitia sekta ya utalii nchini.
Dkt.
Shein alipongeza hatua za maendeleo zilizofikiwa na Mkoa huo katika
sekta za kilimo, utalii, afya, miundombinu na hatua zilizowekwa za
kukabiliana na janga la mabadiliko ya tabia nchi.
Kupitia
majumuisho hayo Dkt. Shein aliwaagiza Mawaziri wa Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar kujenga utamaduni wa kutembea vijijini kwa lengo
la kuwaelimisha wananchi juu ya fursa zinazopatikana katika wizara hizo
ili wananchi wazifahamu na kuzichangamkia.
“
Bado kuna wananchi hawajui kama serikali ina mfumo wa uwezeshaji
unatoa mikopo kwa wajasiriamali na vikundi vingine vyenye malengo ya
kujikomboa kiuchumi, na hadi hivi sasa tayari zaidi ya bilioni mbili
wamekopeshwa wananchi wa maeneo mbali mbali hapa nchini”, alieleza Dkt.
Shein na kuitaka Wizara ya kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto
Zanzibar kutangaza kuwafikia wananchi wa vijijini ili wanufaike na
mfuko huo.
Dkt.
Shein aliwapongeza wakulima wa zao la ndimu ndani ya mkoa huo na
kuitaka Wizara inayohusika na masuala ya kilimo kutumia wataalamu wake
kuwafundishe wananchi mbinu bora za kilimo cha kisasa.
Hata
hivyo alisema licha ya Mkoa huo kupata mafanikio mbali mbali bado
wanatakiwa kuzidisha bidii katika kudhibiti vitendo vya magendo ya
bidhaa mbali mbali vinavyoikosesha serikali mapato.
Dkt.
Shein ambaye pia ni Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar alizindua jengo
la Tawi la CCM Kizimkazi Dimbani ndani ya Mkoa huo, na kuwasihi
viongozi wa chama hicho kutumia vikao vya kikatiba wakati wa kufanya
maamuzi yanayohusu taasisi hiyo badala ya kufanya maamuzi binafsi.
Aliwasihi
wazee wa CCM kuendeleza utamaduni wa kuwafundisha itikadi vijana ili
waweze kujua historia ya chama na nchi ilipotoka kabla na baada ya
mapinduzi ya mwaka 1964.
Aliwambia
wanachama wa chama hicho na wananchi kwa ujumla kuwa Chama cha
Mapinduzi kinapoahidi kinatekeleza kwa wakati kwani miradi yote
inayozinduliwa hivi sasa imetokana na usimamizi mzuri wa Ilani ya
uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2016.
Ziara
hiyo ya siku mbili katika Mkoa wa Kusini, Dkt. Shein alikagua maendeleo
ya ujenzi wa uwanja wa kisasa wa mpira wa miguu katika kijiji cha
Kitogani, alitembelea wajasiriamali wa Saccos ya AMCO na kuona mazao
wanayozalisha yakiwemo Matikiti maji, mihogo, ndimu na Tungule huko
Mtule kijiji cha Paje.
0 comments:
Post a Comment