Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA
S.L.P. 9141,
DAR ES SALAAM.
24/08/2017
TAARIFA KWA
VYOMBO VYA HABARI
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Nyakoro Sirro
amemteua Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Juma Yusuf Ally kuwa Kaimu Kamishna wa
Polisi Zanzibar.
Uteuzi huo unafuatia kustaafu kwa aliyekuwa kamishna wa
Polisi Zanzibar Kamishna Hamdani Omari Makame kwa mujibu wa sheria baada ya
kutimiza umri wa miaka sitini (60).
Kabla ya uteuzi huo DCP Juma alikuwa ni Mkuu wa Utawala na
Fedha Makao Makuu ya Polisi Zanzibar.
IGP Sirro pia amemteua Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Lazaro Mambosasa kuwa Kamanda wa Kanda
Maalum ya Dar es Salaam. Kabla ya uteuzi huo, SACP Mambosasa alikuwa Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Dodoma.
Kufuatia uteuzi huo, aliyekuwa Kaimu Kamanda wa Kanda
Maalum ya Dar es Salaam anakwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, na
aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara Kamishna
Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Neema
Mwalimu Mwanga anakwenda Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam.
IGP Sirro pia amemteua aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa
wa Kipolisi Temeke Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Gilles Bilabaye
Mroto kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma na
Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Emmanuel Lukula kwenda kuwa Kamanda wa
Polisi mkoa wa Kipolisi Temeke.
Kabla ya uteuzi huo, ACP Lukula alikuwa Afisa Mnadhimu wa
Polisi mkoa wa Mbeya.
Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi wote kuendela
kushirikiana na Jeshi hilo kwa kufichua taarifa za uhalifu na wahalifu ili kwa
pamoja tuendelee kuiweka Tanzania salama.
Imetolewa na:
Barnabas David Mwakalukwa - ACP
Msemaji wa Jeshi la Polisi
Makao Makuu ya Polisi.
S.L.P
9141
Dar
es Salaam
Baruapepe
habariphq@yahoo.com
0 comments:
Post a Comment