Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na.Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.
Timu ya Simba SC ambao wapo Visiwani
Zanzibar kwaajili ya kuweka kambi hadi Agost 22, 2017, kesho Alhamis
watacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Mlandege SC mchezo ambao
utasukumwa majira ya saa 2:00 za usiku katika uwanja wa Amaan.
Huu ni mchezo wa kwanza kwa timu ya Simba
kucheza Visiwani hapa ndani ya msimu huu mpya ambapo pia itakuwa ni
mchezo wake wa tano wa kirafiki kufuatia kucheza michezo minne.
Simba walicheza mechi mbili walipokwenda
Afrika ya Kusini kuweka kambi ambapo walifungwa 1-0 Orlando Pirate,
kisha wakatoka sare ya 1-1 na Bidvest baada ya hapo wakaichapa Rayon
Sport ya Rwanda 1-0 kwenye mchezo wa siku ya Simba uliopigwa uwanja wa
Taifa Dar es salam na mwisho kuwafunga Mtibwa Sugar 1-0.
Kwa upande wa Mlandege Jumapili iliyopita
ya Agost 13 walichapwa 2-0 na Yanga kwenye uwanja huo huo wa Amaan
ambapo kesho watakipiga tena na Simba.
0 comments:
Post a Comment