Home » » MAGARI MAZEE FURSA YA UTALII

MAGARI MAZEE FURSA YA UTALII

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
  view-source:http://m.ippmedia.com/sites/default/files/styles/image660/public/articles/2017/08/27/MAGARI%20YA%20ZAMANI.JPG?itok=mWzL3YK8&timestamp=1503829087
MWENYEKITI wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar, Sabah Saleh Ali, amesema maonyesho ya magari ya zamani ambayo yalikuwa yakitumika wakati wa ukoloni ni fursa nzuri ya kukuza utalii wa Zanzibar.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa maonesho hayo yaliyofanyika visiwani Zanzibar, Mwenyekiti huyo alisema maonyesho hayo ni fursa nzuri ya kuutangaza utalii na kuitangaza historia ya Zanzibar kupitia maonyesho hayo.

Alisema Zanzibar inategemea sekta ya utalii katika kukuza uchumi wake, hivyo ni fursa nzuri iwapo maonyesho hayo yataendelezwa kwani yatawavutia wageni wengi zaidi.

“Haya magari ni magari ya kizamani ambayo yalikuwa yakitumiwa enzi hizo miaka ya 1950, kwa kweli nimefurahi sana kuona historia inajirejea,” alisema Mwenyekiti huyo.

Aliwapongeza waandaaji wa maonyesho hayo ambao ni wawekezaji katika sekta ya utalii kwa kuanzisha maonyesho ya magari ya kihistoria ambayo yatasaidia kuenzi na kudumisha historia na vitu vya kale.

Meneja wa hoteli ya Patk Hayat ambaye ndiye mwandaaji wa maonyesho hayo, Garry Friend, alisema wanashukuru kuyafanikisha na yatasaidia kuinua mapato ya nchi kupitia sekta ya utalii.

Alisema wanatarajia kuyaendeleza maonyesho hayo na kuyaboresha zaidi, ili kuitangaza Zanzibar kihistoria na kukuza uchumi wa nchi kupitia sekta ya utalii.

“Huu ni mwanzo tu, leo tumeanza na maonyesho ya magari haya manne ambayo ni magari ya kizamani yaliyokuwa yakitumiwa na wakoloni, lakini imani yetu zaidi mwakani tutakuwa na magari mengi zaidi,” alisema.
Chanzo:Nipashe

0 comments:

Post a Comment

 
Support by Blogs za Mikoa Tanzania
Copyright © 2012. Zanzibar Yetu - All Rights Reserved
Designed by by Blogs za Miikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa