Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akionesha Ramani ya Ujenzi wa Mji wa kisasa utakaojengwa sambamba na ufukiaji wa Bahari ya Eneo la pwani ya Gulioni katika kikao cha siku moja kilichojumuisha Uongozi wa Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Usafirishaji pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Nyumba na Uongozi wa Shirika la Nyumba katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja
Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Nyumba wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) wakati alipofanya kikao cha siku moja pamoja na Uongozi wa Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Usafirishaji katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.
Na Rajabu Mkasaba, IKULU
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,
amesema kuwa kuwepo kwa mabadiliko makubwa ya kimaendeleo baada ya
kuundwa kwa Mamlaka ya Viwanja vya ndege vya Zanzibar kumeweza kuongeza
mapato na kuahidi kuimarika zaidi hali hiyo ndani ya kipindi chake cha
uongozi.
Dk.
Shein aliyasema hayo leo, alipokutana na uongozi wa Wizara ya Ujenzi,
Mawasiliano na Usafirishaji, Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Viwanja
vya Ndege pamoja na Uongozi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege katika vikao
vinavyoendelea Ikulu mjini Zanzibar.
Dk.
Shein alitumia fursa hiyo kuipongeza Mamlaka hiyo kwa kufanya
mabadiliko makubwa katika viwanja vya ndege vya Zanzibar hatua ambayo
imeweza kusaidia kwa kiasi kikubwa ongezeko la mapato katika viwanja
hivyo.
Katika
maelezo yake Dk. Shein alisema kuwa licha ya baadhi ya changamoto
zilizopo lakini Mamlaka imeweza kupata mafanikio makubwa na hivi leo
viwanja vya ndege Unguja na Pemba viweza kuimarika na kuleta tija kwa
kuongeza mapato.
Akizungumza
suala zima la fidia kwa wananchi waliojenga pembezoni mwa uwanja wa
ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar Dk. Shein alisema kuwa
ni vyema likatafutiwa ufumbuzi kwa kuwatafuta wahusika na kuwasikiliza
madai yao ili hatua za malipo ziendele kuchukuliwa.
Akizungumza
na uongozi wa Wizara hiyo kupitia Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la
Nyumba pamoja na Uongozi wa Shirika hilo, Dk. Shein alisisitiza haja ya
Shirika hilo kuzitambua na kuziorodhesha ili kujua idadi ya nyumba zao
zote za Unguja na Pemba pamoja na zile za Wakala hatua ambayo pia,
itasaidia kuepusha udanganyifu.
0 comments:
Post a Comment