Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mkuu wa Skuli ya Uunguzi na
Ukunga Chuo Kikuu cha Aga Mjini Nairobi Kenya Khan Prof. Sharon Brownie
akizungumza na viongozi wa wauguzi na wakunga wa Hospitali Kuu ya
Mnazimmoja akisisitiza juu ya kuinua na kuimarisha kada hiyo kupitia
Jumuia zao.
Mkuu wa Skuli ya Uunguzi na
Ukunga Chuo Kikuu cha Aga Mjini Nairobi Kenya Khan Prof. Sharon Brownie
akizungumza na viongozi wa wauguzi na wakungu wa Hospitali Kuu ya
Mnazimmoja akisisitiza juu ya kuinua na kuimarisha kada hiyo kupitia
Jumuia zao.
Mwenyekiti
wa Jumuia ya Wauguzi na Wakunga Zanzibar Bi. Amina Abdulkadir akitoa
ufafanuzi kuhusu Jumuia hiyo inavyofanyakazi na kusisitiza umuhimu wa
wafanyakazi wa kada hiyo kujiendeleza katika mkutano huo uliofanyika
Hospitali Kuu ya Mnazimmoja
Mmoja wa viongozi wa wauguzi Bi. Salama Rashid Haroub akitoa mchango wake juu ya kuikuza kada ya uuguzi na ukunga Zanzibar.
Baadhi
ya viongozi wa Wauguzi na Wakunga wakifuatilia mkutano mkutano huo
uliohutubiwa na Mkuu wa Skuli ya wakunga na wauguzi kutoka chuo Kikuu
cha Aga Khan Mjini Nairobi Kenya.
Picha
ya pamoja ya viongozi wa wauguzi na wakunga wakiwa pamoja na Mwenyekiti
wa Jumuia ya Wauguzi Zanzibar na wageni wao kutoka Chuo Kikuu cha Aga
Khan Nairobi Kenya ambapo wamekuja Zanzibar kuinua kada ya wakunga na
wauguzi.
Picha na Makame Mshenga.
Na Miza Kona Maelezo
Wauguzi
na Wakunga nchini wamesisitizwa kuongeza bidii katika kuongeza
taaluma katika fani yao kwa lengo la kutoa huduma kwa ufanisi wakati
wa kutekeleza majukumu yao.
Hayo
yameelezwa leo huko Hospitali ya Mnazi Mmoja na Mkuu wa Skuli ya
Wauguzi na Wakunga wa Chuo Kikuu cha Aga Khan nchini Kenya Profesa
Sharon Brownie alipokuwa akizungumza na wasimamizi wa wauguzi na
wakunga wa Hospitali hiyo.
Prof.
Sharon amesema wauguzi wana nafasi muhimu kwa jamii hivyo ni vyema
kutafuta ujuzi kupitia sehemu nyengine kwa lengo la kukuza fani hiyo.
“Asilimia
90 ya wauguzi duniani ni wanawake, wauguzi mnatakiwa kuangalia mitandao
ya wauguzi ambayo inatoa taaluma ya uuguzi kufanya hivyo mtaweza
kubadilika kifanisi katika kazi hii ya uuguzi,” alieleza Profesa Sharon
Alifahamisha
kuwa fani ya uuguzi inatakiwa kufanyakazi kwa kujituma na mashirikiano
katika utendaji na utoaji huduma na kuweza kuinua afya kwa jamii
Alieleza
lengo la ziara hiyo ni kuinua na kuboresha Wauguzi pamoja na Jumuiya za
Wauguzi kwa dhamira ya kuendeleza kitaaluma na kutekeleza majukumu ya
kazi hiyo kwa ubora pamoja na kuimarisha afya kwa jamii.
Nae
Mwenyekiti wa Baraza la Wakunga na Wauguzi Bi Amina Abdulkadir
amewataka wasimamizi pamoja na wauguzi kufanya kazi kwa kujiamini,
kujiheshimu pamoja na kubadilika kifanisi na kujua majukumu ili kuweza
kutekeleza majukumu yao bila ya katawaliwa na kudharauliwa na wengine.
“Muuguzi
anatakiwa kufanya kazi kwa kujiamini, awe smati, ajiheshimu pia
anatakiwa kubadilika kielimu sio awe regerege awe ni mwenye kufanya
maamuzi ndio mfanyakazi mwengine nae atamuheshimu, sisi tunataka
wauguzi muwe juu zaidi katika fani hii,” alifahamisha Bi Amina.
Aidha
Bi Amina amewasisistiza wauguzi hao kuipenda kazi yao kwa lengo la
kutoa huduma iliyo bora kwa jamii ili kuepukana na usumbu na malalamiko
yanayotolewa na jamii.
Nao
wauguzi hao walisema wanafanyakazi katika mazingira magumu
hivyo wanahitaji kupatiwa elimu na vifaa vya afya ili waweze
kujiimarisha zaidi na kutoa huduma bora kwa jamii.
Aidha
wauguzi hao walisisitiza kufanya utafiti katika kazi zao ili kuweza
kujua na kupata sababu zinazoikumba jamii wakati wa utoaji huduma kwa
lengo la kuimarisha afya na kuepukana na changamoto zinanajitokeza.
0 comments:
Post a Comment