Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mhe. Mmanga Mjengo Mjawiri akipokea Cheti cha
Shukrani kutoka kwa Raisi wa Taasisi ya Rafiki Network Bw. Hamad Hamad huko Ofisinini kwake
Mazizini.
Naibu waziri wa Elimu na mafunzo ya Amali wa Zanzibar Mh. Mmanga Mjengo Mjawiri amepokea Cheti cha shukrani
kutoka kwa Taasisi ya Rafiki Network kutokana na juhudi na mchango wake mkubwa aliotoa katika
kufanikisha Bonanza la kihistoria la kimichezo lililoandaliwa na taasisi hiyo kisiwani Pemba.
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa cheti na Rais wa Taasisi ya Rafiki Network Bw. Hamad Hamad
ofisini kwake Mazizini nje kidogo ya mji wa Zanzibar, Mh Naibu Waziri amesema ipo haja ya kufufua
michezo iliyosahauliwa ya Kipemba ili kuibua burudani ambazo amesema kwasasa zimekua adimu.
“Watu wanataka burudani kwasababu zimekua adimu hivyo ni vizuri kuendelea na kufufua michezo
iliyosahauliwa ikiwemo michezo ya kivita ya kipemba (martial arts) kama vile Ngware na Kirumbizi”
Amesema Mh. Mmanga.
Akielezea juu ya kuridhishwa kwake na juhudi za Taasisi ya Rafiki Network katika kuandaa na kusimamia
Tamasha la kimichezo kisiwani Pemba lijulikanalo kama “Pemba Weekend Bonanza”, Mheshimiwa Naibu
Waziri amesema Taasisi ya Rafiki Network imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuamsha hisia za watu
kiburudani zinazohusiana na michezo yao ya kiasili.
Aidha Mh. Waziri amesema burudani zimekua adimu kisiwani Pemba ambapo ametumia kigenzo cha
wananchi kujitokeza kwa wingi katika tamasha la Pemba Weekend Bonanza kuwa ni ishara tosha ya
kuadimika kwa michezo na burudani kisiwani Pemba. Ameongeza kua michezo ni muhimu sana kwa
kuwaunganisha watu.
Taasisi ya Rafiki Network iliandaa tamasha kubwa la Kimichezo Kisiwani Pemba ambalo lilifanyika
kuanzia tare 28 hadi 30 Julai ambapo michenzo mbalimbali ikiwemo mchezo wa Ng’ombe, Resi za
Baiskeli, Mashindano ya Kuogelea na Resi za Ngalawa yalifanyika ambapo washindi na washiriki
walizawadiwa.
0 comments:
Post a Comment