Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akiwaonyesha wajumbe walioshiriki Kongamano la kwanza la Kimataifa la Kamisheni ya Kiswahili ya Afrika Mashariki mpango mkakati wa miaka mitano wa Kamisheni hiyo (kulia) Mtendaji Mkuu wa Kamisheni Prof. Kenneth Simala na (kushoto) Rais Mstaafu wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi.
Maryam Kidiko na Mwashungi Tahir-Maelezo Zanzibar.
KUANDALIWA
kwa kongamano la kwanza la Kimataifa la Kamisheni ya Kiswahili ya
Afrika Mashariki ni miongoni mwa juhudi za kuendeleza lugha ya Kiswahili
katika ukanda huo na Duniani kwa jumla.
Hayo
ameyasema Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia
Suluhu Hassan wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Kamisheni ya Kiswahili
ya Jumuiya ya Afrika Mashariki huko katika ukumbi wa Hoteli ya Golden
Tulip iliopo Malindi Mjini Zanzibar.
Alisema
kongamano hilo lililowashirikisha wataalamu wa lugha ya Kiswahili wa
nchi wananchama wa Afrika Mashariki lina umuhimu mkubwa katika historia
ya maendeleo ya Kiswahili duniani pamoja na kupanga mikutano na
kubadilishana utalaamu .
Hivyo Alieleza kuwa ni muhimu kwa kamisheni kusimamia kwa makini hadhi
ya Kiswahili kama lugha ya mawasiliano ikitambuwa kwamba ukanda wa
Afrika Mashariki ni sehemu ya Dunia yenye lugha tofauti.
Samia
alisema uratibu na uendelezaji wa Maendeleo na matumizi ya Kiswahili
utaimarisha mchakato na utengamano wa Jumuiya kwa maendeleo endelevu.
“Utengamano wa Jumuiya sio tukio bali ni mchakato ambao unapaswa
kuendeshwa na watu wenye kuelewa vizuri matumizi endelevu ya Kiswahili
“Alisema Makamo wa Rais.
0 comments:
Post a Comment