Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Rans Nassor Salim Khamis inayojenga vituo 15 vya afya vya Mradi wa Orio alipotembelea kituo cha Kiboje wa pili (kulia) Meneja Ujenzi wa Kampuni ya Rans Ali Nassor.
Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akitembelea ujenzi wa kituo kipya cha afya Kiboje akiambatana na Mkuu wa Wilaya ya Kati Mashavu Sukwa (kushoto) meneja wa Ujenzi wa Kampuni ya Rans Ali Nassor.
Meneja wa Ujenzi wa Kampuni ya Rans Ali Nassor akimpa maelezo Waziri wa Afya juu ya ukarabati wa kituo cha afya cha Uroa alipofanya ziara ya kutembelea vituo vya Mradi wa Orio.
Muonekano wa kituo kipya cha afya cha Kijini Matemwe kinachojengwa kwa ushirikiano wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Uholanzi kupitia Mradi wa Orio.
Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kijini Matemwe baadaya kuangalia maendelea ya ujenzi wa kituo kipya cha afya cha kijiji hicho.
Na Ramadhani Ali – Maelezo
Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar inaendeleza dhamira yake ya kuleta mabadiliko
makubwa katika sekta ya afya kwa kuimaisha huduma za afya na kujenga
vituo vyenye hadhi vijijini.Dhamira hiyo inaendelea kutekelezwa kwa
pamoja na wafadhili wa maendeleo wanaunga mkono juhudi zinazochukuliwa
na Serikali katika kufikiaq malengo hayo.
Waziri
wa Afya Mahmoud Thabit Kombo ameeleza hayo alipotembelea vituo vitatu
vipya vya afya vya Kiboje, Kijini Matemwe na Chaani kubwa na kituo cha
Uroa kinachofanyiwa ukarabati mkubwa.Amesema serikali ya Uholanzi kwa
kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia mradi wa Orio
hivi sasa unaendelea na ujenzi wa vituo 15 vya afya nane vikiwa
vinajengwa Unguja.
Waziri
Mahmoud aliwaeleza wananachi wa sehemu hizo kuwa lengo la kujengwa
vituo hivyo nikuwasogezea huduma za afya karibu na sehemu wanazoishi na
kupunguza msongamano wa wagonjwa katika Hospitali kuu za
mijin.Amewahakikishia wananchi kuwa vituo vinavyojengwa kupitia mradi wa
Urio vitakapomalizika vitakuwa na vifaa vya kisasa na vitatoa huduma
zote muhimu zikiwemo wodi za kujifungulia.
Aliongeza
kuwa Wizaara ya Afya inajiandaa kuhakikisha kuwa vituo vyote
vinavyojengwa vinakuwa na wafanyakazi wa fani zote muhiumu ili
kuwapunguzia shida.“Wananchi wa Kijini kituo chenu ambacho ni cha
daraja la pili kitakapomalizika kitatoa huduma zote muhimu na wagonjwa
watatoka mjini kuja kutafuta matibabu hapa,”Waziri aliwahakikishia.
0 comments:
Post a Comment