Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Rais wa Chama cha Madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania Dokt,Lorna Carneiro kulia akitoa hotuba ya makaribisho katikaUfunguzi wa Zoezi la Uchunguzi wa Maradhi ya kinywa na Meno katika Kituo cha Afya Rahaleo Mjini Unguja.
Mkurugenzi wa Kinga na Elimu ya Afya katika Hospitali ya Mnazi mmoja Dkt,Fadhil Abdalla akitoa hotuba ya Ufunguzi wa Zoezi la Uchunguzi wa Maradhi ya Kinywa na Meno katika Kituo cha Afya Rahaleo Mjini Unguja.Zoezi linalofanywa na Chama cha madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania(TDA).wakishirikiana na madaktari wa Zanzibar.
Mkurugenzi wa Kinga na Elimu ya Afya katika Hospitali ya Mnazi mmoja Dkt,Fadhil Abdalla katikati akiwa katika picha ya pamoja na Madaktari kutoka Chama cha madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania(TDA).pamoja na madaktari wa Zanzibar katika Zoezi la Uchunguzi wa Maradhi ya Kinywa na Meno katika Kituo cha Afya Rahaleo Mjini Unguja.
Na Khadija Khamis –Maelezo
Jamii
inatakiwa kuweka utaratibu wa kupima afya ikiwemo afya ya kinywa na
meno ili kupatiwa uchunguzi wa awali pamoja na elimu sahihi ya afya
angalau mara mbili kwa mwaka .
Hayo
aliyaeleza na Mkurugenzi wa Kinga na Elimu ya Afya Dr Fadhil Mo’hd
Abdalla huko katika Kituo cha Afya Rahaleo, wakati akifungua zoezi la
uchunguzi wa afya ya kinywa na meno linaloendeshwa na Chama cha
Madaktari wa Kinywa na Meno kutoka Tanzania .
Alisema
afya hiyo ni muhimu kufanyika awali kabla ya madhara, kwa kupatiwa
ushauri wa mapema kabla ya athari kujitokeza na kusababishwa kupoteza
meno .Alifahamisha
kuwa katika miaka ya nyuma elimu ya afya ya kinywa na meno zilikuwa
zikitolewa katika maskuli ,wataalamu hutoa elimu kwa wanafunzi pamoja
na kung’oa meno kwa wale ambao meno yao yameadhirika .
Aidha
alisema mpango huo wa uimarishaji afya ya jamii iko haja kurejea
utaratibu wa kizamani , wataalamu wa afya ya kinywa na meno kutoa
huduma za matibabu katika maeneo mbali mbali ikiwemo maeneo ya maskuli
na vijijini .
“Huu
usiwe mwanzo wa kuonyesha njia kwa jamii na wala msisubiri kuumwa
kila muda mujiwekee utaratibu wa kujichunguza afya zenu ikiwemo afya ya
kinywa na meno pamoja na maradhi yasioambukiza ili muweze kupata ushauri
mapema kwa Madaktari ,”alisema Mkurugenzi Kinga.
0 comments:
Post a Comment