Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Zanzibar Dkt Ghirmay Andemichael akitoa maelezo ya Shirika hilo kwenye warsha ya siku tatu ya kuimarisha kanuni za kupambana na matumizi ya tumbaku inayofanyika Hoteli ya Golden Tulip Malindi Mjini Zanzibar.
Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Jamala Adam Taib akifungua warsha ya kuimarisha kanuni za mapambano ya matumizi ya bidhaa zinazotokana na tumbaku katika Hoteli ya Golden Tulip Malindi Mjini Zanzibar.
Dkt. William Maina kutoka WHOAFRO akitoa maelezo ya Azimio la WHO na sheria za kimataifa dhidi ya mapambano ya matumizi ya bidhaa zinazotokana na tumbaku katika warsha ya kuimarisha kanuni za mapambano hayo katika Hoteli ya Golden Tulip Malindi.
Baadhi ya washiriki wa warsha ya kumiarisha mikakati ya kanuni za kupiga vita matumizi ya tumbaku inayofanyika Hoteli ya GoldenTulip Malindi Mjini Zanzibar.
Picha ya pamoja ya mgeni rasmi na washiriki wa warsha ya kuimarisha mikakati ya kupiga vita matumizi ya tumbaku inayofanyika Hoteli ya Goden Tulip Malindi Mjini Zanzibar.Picha na Makame Mshenga.
Na Ramadhani Ali - Maelezo.
Wizara
ya Afya Zanzibar inaendelea kuimarisha kanuni za kupunguza matumizi ya
tumbaku baada ya kuundwa sheria ya Afya ya Jamii ya mwaka 2012 na
kuridhia Azimio la Shirika la Afya ulimwenguni (WHO) kupiga vita bidhaa
zinazotokana na tumbaku katika kunusuru afya za wananchi.
Mkurugenzi
Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Jamala Adam Taib amesema Wizara hiyo tayari
imeweka kanuni ya kukataza kuvuta sigara kwenye mikusanyiko ya watu
katika kuwanusuru waathirika wa moshi wa sigara bila ya kuwa wavutaji.
Dkt.
Jamala ameeleza hayo alipokuwa akifungua warsha ya siku tatu ya
kuimarisha kanuni za kupambana na matumizi ya tumbaku katika Hoteli ya
Golden Tulip iliyopo Malindi iliyowashirikisha wadau kutoka taasisi
mbali mbali za Serikali.
Mkurugenzi
Mkuu alisema uvutaji wa sigara umeonekana kuwa chanzo kikubwa cha
ongezeko la maradhi yasiyoambukiza ikiwemo saratani, sukari maradhi ya
mapafu na maradhi ya ini.Alisema pamoja na kwamba
Zanzibar haizalishi tumbaku na haina viwanda vinavyohusika na bidhaa za
tumbaku bado wananchi wamekuwa waathirika wa moshi wa sigara.
Alieleza
kuwa tafiti zilizofanyika zinaonyesha kuwa asilimia kubwa ya watu
wanaofariki kutokana na maradhi hayo yanatokana na kuvuta sigara ambapo
asilimia 15 ya vifo hivyo vinawafika watu wanaovutishwa moshi na
wavutaji wa sigara bila ya wao kushiriki kuvuta.
Katika
kufanikisha lengo hilo Dkt. Jamala alizishauri taasisi za Serikali,
Jumuiya za kiraia na jamii kwa jumla kuunga mkono kanuni inayokataza
sigara kuvutwa kwenye mikusanyiko ya watu na nyengine zinazoundwa ili
kulinda afya zao.
Mwakilishi
wa WHO Zanzibar Dkt. Ghirmay Andemichael alisema Zaidi ya watu milioni
saba wanapoteza maisha kila mwaka duniani kutokana na matumizi ya bidhaa
zinazotokana na tumbaku ambapo asilimia 80 ya vifo vinatokea katika
mataifa yanayoendelea.
0 comments:
Post a Comment