Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Bi. Harusi Said Suleiman akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Bohari kuu ya Dawa Zahran Ali Hamad alipotembea kuona dawa katika bohari hiyo, iliyopo Maruhubi Mjini Zanzibar.Picha na Makame Mshenga.
Na Mwashumgi Tahir Maelezo Zanzibar
SERIKALI
ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Afya Zanzibar
imewahakikishia wananchi kuwa Bohari kuu ya Dawa inadawa za kutosha za
kuhudumia wagonjwa wanaofika kupata matibabu katika Mahospitali na vituo
vya Afya.
Kauli
hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Afya Harusi Said Suleiman wakati
alipofanya ziara katika Bohari kuu ya Dawa na kuangalia namna ya
upatikanaj i wa dawa.
Amesema
uwepo wa Dawa katika Bohari kuu ya dawa nikuonesha kuwa Serikali ina
imani na wananchi wake kwa kuongeza Bajeti ya ununuzi wa dawa kwa
asilimia mia moja ambapo upungufu upo kidogo kwenye dawa za wagonjwa wa
akili ambap o Wizara iko mbioni kutatua tatizo hilo.
”‘Wananchi
msininuwe dawa katika mahospitali na vituo vya Afya zipo za kutosha
kwani Serikali imefanya jitihada kubwa ya kueneza dawa na kuzisambaza
mahosptalini mote na vituo vya afya ambapo kama kutakuwa na upungufu
wa dawa Wizara tutatoa taarifa maalum kwa wananchi wake”. Naibu Waziri
huyo Alisisitiza.
Amewataka
wafanyakazi wa Mahospitalini na Vituo vya Afya kuagiza dawa kwa wakati
kwani kufanya hivyo kutasaidia kuondosha urasimu kwa wagonjwa ambao
wanaokwenda kupata huduma ya matibabu na kuwambiwa dawa hakuna ambapo
kuna dawa za kutosha katika Bohari ya dawa.
Kwa
upande wa Mkurugenzi Bohari kuu ya Dawa Zahran Ali Hamad amesema kwa
mujibu wa mahitaji ya dawa muhimu zinazotumika katika visiwa vya Unguja
na Pemba dawa zipo za kutosha kwa kuwahudumia wananchi.
Amezitaja
dawa hizo ni pamoja na za akinamama wanofika kujifungua,dawa za mpango
wa uzazi, dawa ya kisukari na pressure na maradhi mengine na
kuwasisitiza wahudumu wa afya kuagiza dawa kwa wakati.
0 comments:
Post a Comment