Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Khadija Khamis – Maelezo
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe, Issa Haji Gavu amewataka Watumishi Wahudumu wa Viongozi wa Serikali na Wageni kuitumia vizuri fursa ya mafunzo walioipata ili kuzidisha ufanisi katika kazi zao .
Alisema ikiwa
wataitumia vyema vizuri fursa hii katika kujipatia mafunzo ya upishi
na ukarimu wataongeza utaalamu na kuweza kupata mbinu zaidi ya
kubadilishana uzoefu kwa namna moja au nyengine .
Hayo aliyasema
katika ufunguzi wa mafunzo ya wiki moja ya watumishi wahudumu wa
Viongozi wa Serikali uliofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Habari
Utalii Utamaduni na Michezo Kikwajuni yatayoendeshwa na Serikali ya
Jamhuri ya Watu wa China (China National research Institute of food and
Fermation Industries).
Aidha
alisema mafunzo hayo yatarahisisha kutafsiri nadharia halisi
zitazofundishwa na kuona uhalisia wa mambo yanavyokuwa pamoja na
kubadilishana uzoefu na kuzidisha ushirikiano .
Aliwataka
washiriki kuwa makini katika kuzingatia muda wote wa masomo pamoja na
kutoa mashirikiano kwa wakufunzi ili waweze kuwa na ari ya ufundishaji
pia wasisite kuuliza maswali iwapo watakuwa hawajafahamu, ili lengo la
mafunzo hayo yafanikiwe.
“Wengi wenu bado
mna umuhimu wa kutafuta elimu hasa mkizingatia kwamba elimu haina
mwisho na ndio dira ya mafanikio katika kulipeleka mbele Taifa hasa
katika wakati huu wa sayansi na teknolojia.” alisema Waziri.
Alifahamisha
jinsi ya makubaliano ambayo yaliofikiwa na Viongozi wa Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar Na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kwa
kuwapatia mafunzo watendaji wake ya upishi na ukarimu iwe chachu ya
kujipatia maendeleo kwa jamii .
“Faraja urafiki
na uhusiano uliodumu kwa muda mrefu uendelee kudumu baina ya
Ndugu zetu hao wa Serikali hizo, “alisema Waziri Gavu .
Hata hivyo alitoa
rai kwa wakufunzi hao kuweza kujifunza mambo mbali mbali ya kihistoria
hapa Zanzibar na kutembelea sehemu za kivutio pamoja na kuona miti
ambayo ni maarufu kwa viungo ambavyo vinatumika Zanzibar .
Nae Balozi Mdogo
wa Jamhuri ya Watu wa China Xie Xiaowi alisema wataendelea kudumisha
mashirikiano baina yao pamoja na udugu wao ili kuleta maendeleo ya
kiuchumi na kiutamaduni katika nchi hizo .
Nae mmoja wa
washiriki wa mafunzo hayo Mvita Khamis alisema amefurahishwa kupata
fursa hiyo ya mafunzo ya mapishi na ukarimu anatarajia
akimaliza atayatumia ipasavyo kwa uweledi mkubwa katika kutoa huduma
bora kwa Viongozi na wageni .
0 comments:
Post a Comment