Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa huduma za nishati na maji Zanzibar
(ZURA) Haji Kali Haji akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na
hali ya upatikanaji wa mafuta Zanzibar huko Ofisini kwake Maisara
Zanzibar (picha na Kijakazi Abdalla –Maelezo)
Na Mwashungi Tahir Maelezo Zanzibar
MKURUGENZI
Mkuu Mamlaka Ya Udhibiti Wa Huduma Za Nishati Na Maji Zanzibar(ZURA)
Haji Kali Haji aliwataka wananchi kuondoa wasiwasi kuhusu tatizo la
upungufu wa mafuta nchini kuwa yapo ya kutosha.
Alisema
mafuta yapo ya kutosha ingawa kwa siku mbili kulijitokeza upungufu wa
mafuta aina ya dizeli na hii ni kutokana na kazi ya usambazaji katika
wa mafuta hayo katika vituo.
Akizungumza
na waandishi wa habari hizi huko ofisini kwake Maisara amesema wananchi
hawatokuwa na tatizo hilo kwa upande wa dizeli na kuahidi baada ya siku
mbili tatizo hili litaondoka kabisa.
“
Hali ya sasa ya mafuta hapa Zanzibar itaendelea kuweko na
hawategemei kuadimika badala ya kuwepo mafuta ya kutosha na kuweza
wananchi kujipatia huduma hii bila usumbufu”Alieleza mkurugenzi huyo.
Aidha
alisema kwa upande wa Kampuni ya GAPCO mafuta aina ya dizeli yapo
lita 39,112 na vile vile watapokea mafuta mengine yaliyokuwa ya kampuni
Zanzibar Petrolium (ZP) LITA 168,000 za dizeli.
Pia
amesema kwa upande wa Petrol kampuni hiyo ya Gapco ina lita 405,000, na
kwa upande wa Kampuni United Group kwa mwezi huu wa Septemba ina lita
2,267,000 za Petrol na lita 1,91,424 za mafuta aina yaq dizeli na
mafuta ya taa lita 629,000.
Kwa
upande wa kampuni ya Zanzibar Petrolium (ZP) Mkurugenzi amesema lita
7,000,00 za Petrol wakati Dizeli kampuni hiyo ina lita 800,000 na kwa
upande wa mafuta ya taa wana lita 250,000.
Akiendelea
kwa kusema katika mwezi wa Oktoba Kampuni ya ZP watakuwa na lita
1,200,000 za Petrol wakati mafuta ya dizeli watakuwa na lita 800,000 na
mafuta ya taa lita 250, 000.
Amesema
kwa kipindi hiki cha miezi miwili Kampuni ya AUGUSTA ENERGY kutoka
Switzerland iliyoshinda zabuni ya uletaji mafuta Zanzibar itaingiza
mafuta jumla ya lita 9,57,116 za Petrol na lita 7,867.538 za mafuta aina
ya dizeli.
Na kwa upande wa Pemba , MT Ukombozi ilishusha mafuta lita 360,000 za dizeli na lita 400,000za mafuta ya Petrol.
Mkurugenzi huyo amesema kwa upande wa mafuta ya ndege Kampuni ya PUMA imeingiza jumla ya lita 2,300,000 kwa mwezi huu .
Pia
amewahakikishia wananchi kuwa hawatopata usumbufu tena tayari Kampuni
ya AUGUSTA ENERGY imeleta mafuta ya ziada tani 200 za Petrol na tani
150 za Dizeli mafuta ambayo kwa sasa yamo katika meli hiyo ikiwa ni
ziada ya yale wanayotakiwa kuleta Zanzibar.
0 comments:
Post a Comment