Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Salum Vuai, MAELEZO
UJUMBE
wa Serikali ya Oman uliokuwepo Zanzibar tangu Oktoba 12, 2017, leo
umebariki maandalizi ya matengenezo makubwa ya jengo la kihistoria Beit
El Ajaib lilioko Forodhani katika
Mji Mkongwe wa Zanzibar.
Ujumbe
huo ukiongozwa na Waziri wa Mafuta na Gesi wa Oman Dk. Mohammed Hamad
Al Rumhy, umelitembelea jengo hilo ukiambatana na baadhi ya viongozi wa
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kukagua hali yake halisi.
Lengo
la ziara hiyo lilikuwa kuweka jiwe la msingi kama ishara ya maandalizi
ya matengenezo hayo chini ya ufadhili wa Serikali ya Oman inayoongozwa
na Sultan Qaboos bin Said, yanayotarajiwa kuanza wakati wowote kutokea
sasa. Jengo la Beit El Ajaib lililojengwa mwaka 1883 wakati wa utawala
wa Sultan wa pili wa Zanzibar Barghash bin Said, limeachwa kutumika kwa
miaka kadhaa sasa kutokana na kukabiliwa na uchakavu mkubwa ikiwemo
kuanguka baadhi ya kuta zake.
Beit
El Ajaib ni miongoni mwa vivutio vikubwa vya utalii hapa Zanzibar, na
kabla kuzuiwa matumizi yake, lilikuwa likiingizia mapato serikali kwa
kutembelewa na watalii wengi kutoka nchi mbalimbali duniani.
Matengenezo
hayo yanatarajiwa kulijejeshea haiba jengo hilo ambalo ni miongoni mwa
vivutio vikubwa vya utalii humu visiwani, na kuanza kutumiwa tena wa
shughuli za kitalii. OKTOBA 2017
0 comments:
Post a Comment