Home » » ZANZIBAR KUADHIMISHA SIKU YA MTOTO NJITI NOVEMBA 17 /2017

ZANZIBAR KUADHIMISHA SIKU YA MTOTO NJITI NOVEMBA 17 /2017

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

 Katibu Mkuu Wizara ya Afya Asha Ali Abdalla akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya mtoto Njiti yatakayofanyika tarehe 17 mwezi, mkutano huo ulifanyika Ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazimmoja Mjini Zanzibar.
 Daktari wa watoto Khamis Ali Abeid akitoa ufafanuzi wa masuala ya waandishi wa habari katika mkutano uliozungumzia maadhimisho ya mtoto njiti yatakayo fanyika tarehe 17 mwezi huu, mkutano huo  ulifanyika Wizara ya Afya Mnazimmoja.
 Muuguzi Maryam Juma Bakari kutoka Hospitali Kuu ya Mnazimmoja akitoa shukrani kwa waandishi wa habari katika mkutano huo.
Waandishi wa habari Makame Mshenga wa Maelezo na Rahma Suleiman wa Gazeti la Nipashe wakifanya zoezi la njia muafaka ya kumpatia huduma ya kumbeba mtoto njiti ili apata joto la mzazi (kangaroo) katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika Wizara ya Afya.Picha na Makame Mshenga.


Na Ramadhani Ali – Maelezo 

Jamii ya wazanzibari  imeshauriwa kufikiria mikakati na huduma bora zitakazosaidia kupunguza idadi ya kuzaliwa na kufariki watoto njiti ili ambao wanakuwa mzigo kwao na Serikali kwa jumla.

Ushauri huo umetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Bi. Asha Ali Abdalla alipokuwa akitoa tamko  kwa waandishi wa habari kuhusu siku ya maadhimisho ya watoto njiti duniani katika ukumbi wa Wizara hiyo Mnazimmoja Mjini Zanzibar.

Alisema sababu ya kufanyika maadhimisho ya watoto njiti duniani sio kuwabeza watoto hao lakini ni kuamsha hisia na kuinua uwelewa kwa wananchi na watoa huduma  ya afya ya watoto hao kwani iwapo hatua zinazofaa hazitachukuliwa wataendelea kuzaliwa na kufariki kwa idadi kubwa.

Alisisitiza kuwa Shirika la Afya duniani linaamini kuwa vifo vya watoto njiti vinaweza kuepukika kwa silimia 75 iwapo jamii ikishirikiana na Serikali wataweka mkazo huduma za kinga, ugunduzi wa matatizo mapema na matibabu bora na kwa wakati stahili.

0 comments:

Post a Comment

 
Support by Blogs za Mikoa Tanzania
Copyright © 2012. Zanzibar Yetu - All Rights Reserved
Designed by by Blogs za Miikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa