Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
Na Mwandishi Wetu
MAKAMU
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi anaondoka Nchini jana
jioni kuelekea Washington kuhudhuria Mkutano wa 15 wa Jumuiya ya
Wafanyabiashara wenye asili ya Afrika ya Kaskazini Magharibi mwa Pacific
unaotarajiwa kufanyika katika Jimbo la Seattle Nchini Marekani.
Balozi
Seif amepata heshima hiyo kufuatia ujumbe wa Jumuiya ya Wafanyabiashara
wenye asili ya Afrika kutoka Marekani uliowahi kufanya ziara hapa
Zanzibar kati kati ya mwezi wa April Mwaka huu na kujionea mazingira
mazuri ya uwekezaji jambo ambalo Zanzibar imepatiwa fursa ya kwenda
kujitangaza Nchini humo.
Mtandao
wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wenye asili ya Afrika Nchini Marekani
umeamua kufungua ukurasa mpya katika kuona inaendeleza mashirikiano na
Nchi rafiki ikilenga kusaidia taaluma na hata uwezeshaji kwa Taasisi na
Mashirika Barani Afrika ili yajinyanyue kiuchumi.
Katika
ziara hiyo ya wiki moja ya Kiserikali itakayotoa pia fursa ya
kutembelea baadhi ya Makampuni na Taasisi za Umma, Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar anauongoza ujumbe wa Viongozi saba wa Serikaliwakiwamo
Mawaziri, Watendaji wa serikali na Maafisa waandamizi.
Viongozi
anaofuatana nao ni Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi, Waziri wa Nchi Ofisi
ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohammed Aboud Mohammed,
Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Mh. Nassor Ahmed Mazrui pamoja na
Mwakilishi wa Jimbo la Kwamtipura Mh. Hamza Hassan Juma.
Wengine
ni Mwenyekiti wa Chama cha wafanyabiashara Zanzibar Abdulla Abass,
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Makazi, Maji na Nishati Ali Khalil Mirza,
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Abdulla Mzee Abdulla,Mkurugenzi Mkuu
wa Mamlaka ya Bahari Kuu Zahor Mohammed El- Kharousy pamoja na timu ya
wafanyabiashara wa Zanzibar.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif na Ujumbe wake akiambatana na
baadhi ya wafanyabaiashara maarufu hapa Zanzibar atapata fursa ya
kutembelea Kampuni ya utengenezaji wa ndege za Abiria na mizigo ya
Baeing Mjini Seattle, kukutana na Uongozi wa Mfuko wa misaada wa Melinda
Gates na ule wa Microsoft pamoja na jumuiya ndogo ndogo za
wafanyabiashara.
Maeneo
mengine watakayopata fursa ya kutembelea ni ni baadhi ya Taasisi za
Serikali, Meya wa Jiji la Seattle ziara iakayoambatana pia na vikao na
Mikutano ya Wafanyabiashara wa Zanzibar na Mji huo katika kubadilishana
mawazo na kuanza kupanga mikakati ya ushirikiano.
Aidha
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amepanga kukutana na Wanachama wa
Jumuiya ya Wazanzibari na Watanzania wanaoishi Mjini Seattle na
Washington kwenye Tafrija maalum waliyojipanga kumuandalia yeye na
ujumbe wake aliofuatana nao.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif anatarajiwa kukamilisha ziara
yake Mjini Seattle Nchini Marekani Mnamo Tarehe 14 Novemba 2013 na
kurejea nyumbani kwa kupitia Dubai.
Mapema
asubuhi kabla ya kuondoka Nchini kuelekea Marekani Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alikutana na Balozi Mdogo mpya wa
Jamuhuri ya Watu wa China hapa Zanzibar Bwana Xie Yunliang ambae alifika
kujitambuluisha rasmi.
Katika
mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Vuga Mjini Zanzibar Viongozi hao walielezea haja ya pande hizo
mbili kuendelea kushirikiana katika miradi ya maendeleo China ikiwa
mshirika mkubwa wa Zanzibar katika uimarishaji uchumi na ustawi wa
Jamii.
Balozi
Xie Yungliang alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba
China itaendelea kuunga mkono harakati z maendeleo za Zanzibar katika
kujiletea maendeleo na kupunguza umaskini.
Amesema
China ilitenga zaidi ya Yuan Milioni Mia moja katika kuunga mkono
miradi ya Skuli, awamu ya Pili ya ujenzi wa uwanja wa ndege bwa
Kimataifa wa Zanzibar Kisauni pamoja na ile awamu ya Pili ya mradi wa
Mkongo wa Mawasiliano hapa Zanzibar.
Naye
akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif
aliipongeza Jamhuri ya Watu wa China kwa jitihada zake za makusudi za
kuona Zanzibar inajikwamua kutoka katika wimbi la umaskini.
Balozi
Seif alimuahidi Balozi huyo Mdogo mpya wa Jamuhuri ya Watu wa China
kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itajitahidi kumpa ushirikiano
wa karibu katika utekelezaji wa majuku yake aliyopamngiwa na Nchi yake.
Baadaye
Balozi Seif pia alifanya mazungumzo na Balozi Mdogo wa Oman hapa
Zanzibar Bwana Saleh Suleiman Al – Harith ambae naye alifika
kujitambulisha bada ya kuteuliwa na Nchi yake kufanya kazi ya
Kidiplomasia hapa Zanzibar.
Mazungumzo
yao yalijikita zaidi katika kuendeleza uhusiano na ushirikiano uliopo
kati ya Nchi hizo ambao ni wa kihistoria kutokana na maingiliano ya
kidamu ya wananchi wa pande hizo mbili.
Balozi
Seif alimueleza Balozi Mdogo wa Oman Nchini kwamba Zanzibar Zanzibar
inahitaji kuwa na viwanda vidogo vidogo hasa vya matunda ilikuweza
kusaidia uchumi wake.
Amesema
wananchi wengi hasa wakulima wamekuwa wakizalisha idadi kubwa ya
matunda ambayo baadaye hupotea na kuleta hasara kutokana na wakulima hao
kukosa utaalamu wa hifadhi ya matunda hayo.
Aliipongeza
Oman kwa misaada yake mikubnwa inayoendelea kutoa kwa Zanzibar katika
Nyanja za za maendeleo ambayo inazidi kuimarisha uhusiano uliopo kati ya
mataifa hayo mawili.
Naye
kwa aupande wake Balozi mdogo wa Oman hapa Zanzibar Bwana Saleh
Suleiman Al –Harith amewapongeza Viongozi na Wananchi wa Zanzibar kwa
ushirikiano waliompa uliomuwezesha kutekeleza majukumu yake vizuri
katika kipindi kifupi cha utumishi wake.
Balozi
Saleh alimuhakikishia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif
kwamba lile ombi la Zanzibar la kutaka mkutano wa ushirikiano wa
wafanyabiashara wa Nchi za Ghuba Oman ikiwa mratibu atalifikisha katika
ngazi zinazohusika wakati ataporejea Nchini mwake.
0 comments:
Post a Comment