Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini
Pemba Mhe Dadi Faki Dadi amelipongeza Shirika la Action Aid kuwa mstari wa
mbele katika mapambano dhidi ya umaskini na utetezi wa uvunjivu wa sheria
juu ya kulinda haki za wanawake Visiwani Zanzibar.
Katika hotuba iliyosmwa na
kwa niaba yake na Afisa Tawala Mkoa huo Mwalim Khamis Salim Mohammed kwenye
maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukandamizaji wa wanawake , amesema kuwa
uwamuzi wa shirika hilo umetoa fursa ya kujenga jamii ya wazanzibar iliyo na
uadilifu .
Aidha amefahamisha kwamba
Serikali nayo kwa upande wake imechukua hatua kukabiliana na matendo hayo ,
ambapo miongoni mwa hatua hizo ni kuanzisha vituo vya mkono kwa mkono pamoja na
madawati ya wanawake .
Amesema kuwa pamoja na
changamoto mbali mbali zinazojitokeza siku hadi siku , ikiwemo
ucheleweshwaji wa kesi mahakamani , rushwa na gharama za kufuatilia kesi lakini
hakuzuii wahalifu kushawishika kuachana na vitendo hivyo .
Nao washiriki wa maadhimisho
hayo wameshauri elimu ya ukatili wa kijinsia na udhalilishaji wa wanawake
na watoto ianze kutolewa maskulini ili kuwajenga uwelewa watoto wa kike jinsi
ya kukabiliana na matendo hayo .
Aidha wameshauri wahusika
wanaofanya suluhu baada ya kesi ya udhalilishaji kufikishwa Polisi wachukuliwe
hatua ili kukomesha kuwepo na tabia hiyo ndani ya jamii .
0 comments:
Post a Comment