TIMU
ya soka ya Taifa ya Zanzibar, ‘Zanzibar Heroes’ jana ilianza vema
michuano ya Kombe la Chalenji baada ya kushinda mabao 2-1 dhidi ya Sudan
Kusini.
Katika
mechi hiyo iliyochezwa kwenye uwanja wa Nyayo, Nairobi kuanzia saa nane
mchana, timu zote zilionekana kushambuliana kwa zamu, lakini Zanzibar
ilionekana kutumia uzoefu kuizidi maarifa timu ngeni kwenye ukanda wa
Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Sudan Kusini.
Zanzibar
ilikuwa ya kwanza kupata bao la kuongoza likifungwa na Suleiman Kassim
Selembe kabla Adeyum Saleh Ahmed hajafunga bao la pili. Sudan ilipata
bao lake la kufutia machozi katika dakika ya 73 likiwekwa kimiani na
Fabiano Elius Lako.
Aidha
mechi nyingine iliyochezwa jana ilikuwa ni kati ya Ethiopia na Kenya
ambapo timu hizo zilitoka suluhu. Kwa upande wa Bara, Kilimanjaro Stars,
leo itakuwa kwenye uwanja wa Machakos ikicheza na timu mwalikwa Zambia.
Kilimanjaro
Stars ina matarajio makubwa ya kushinda mechi hiyo inayotabiriwa kuwa
na ushindani mkubwa kutokana uimara wa Zambia. Mechi nyingine
itakayochezwa leo ni kati ya Burundi na Somalia.

Chanzo;Habari Leo

0 comments:
Post a Comment