Akizungumza na Tanzania Daima wiki iliyopita katika viwanja vya Beit
el tras wakati ya maonesho ya maadhimisho ya Miaka 50 ya Mapinduzi ya
Zanzibar, Ofisa habari wa mamlaka hiyo, Ally Changwila, alisema wakazi
wa Zanzibar wamekuwa wakijitokeza wakiwemo vijana ambao wengi wao
walikuwa na hamu ya kujua namna ya wao kuwa marubani.
Changwila alizitaja sifa za mtu kuwa rubani ni awe angalau na ufaulu
mzuri katika masomo ya Hesabu na Jiografia, awe na ufahamu mzuri wa
lugha ya Kiingereza, afya njema, na awe amesoma kozi ya urubani.
Pia alisema pia awe amefanya mitihani maalumu inayotolewa na TCAA na kupatiwa leseni ya urubani.
Alisema kuna hatua mbalimbali za kusomea kozi za urubani. Zipo hatua
za awali ambazo mafunzo yake yanatolewa hata hapa nchini ambayo mhitimu
akimaliza anakuwa na uwezo wa kurusha ndege binafsi, na hatua nyingine
ni ile ya marubani wenye uwezo wa kurusha ndege za abiria ambayo masomo
yake yanatolewa nje ya nchi ikiwemo Afrika Kusini.
Alisema kitendo cha baadhi ya wakazi hao kuonyesha nia ya kutaka kuwa
marubani ni kizuri, hasa ulizingatia kada hiyo inakua kwa kasi nchini
na uhitaji wa marubani unaongezeka siku hadi siku.
Chanzo;Tanzania daima
0 comments:
Post a Comment