Home » » MADEREVA WAPIGWA STOP KUBEBA KARAFUU

MADEREVA WAPIGWA STOP KUBEBA KARAFUU

Mkuu wa Wilaya ya Wete Bw Omar Khamis Othman amewataka madereva wa gari za abiria na mizigo kuacha tabia ya kubeba karafuu kutoka shehia moja kwenda nyingine  ambazo hazina kibali cha kusafirishia .

Amesema kuwa serikali ya Wilaya hiyo imebaini kuwepo madereva ambao wanakaidi agizo hilo na kuwafanya waendelee kuchukua karafuu kinyume na utaratibu .

Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi kufuatia kukamatwa kwa kijana Khamis Salum Khatib Mkaazi wa Daya Mtambwe  akisafirisha magunia mwawili ya karafuu bila ya kuwa na kibali .

Aidha Mkuu huyo wa Wilaya amebainisha kwamba hata gari zinazotoka harusini nazo zimekuwa zikitumika kubeba karafuu na kuongeza kwamba hawatasita kuchukua hatua kwa gari hata kama ikiwa imebeba harusi .

Bw Omar amewaagiza masheha wote katika Wilaya hiyo kuwa na utaratibu wa kuzigakua gari zote ili kuwadhibiti wananchi ambao wamekuwa wakihuumu uchumi wa nchi kwa kusafirisha karafuu kwa njia ya magendo .

 Hata hivyo amesema kuwa katika msimu wa ununuzi wa karafuu  magendo yamepungua hii ni baada ya wananchi kukubali kutoa taarifa kwenye vyombo vya ulinzi  .

0 comments:

Post a Comment

 
Support by Blogs za Mikoa Tanzania
Copyright © 2012. Zanzibar Yetu - All Rights Reserved
Designed by by Blogs za Miikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa