Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, imesema shehena ya magogo
yaliyokamatwa yakiingizwa nchini kwa njia ya magendo yakitokea
Madagascar yatarejeshwa nchini humo, kwa sababu Zanzibar haina sheria ya
misitu ya kuwashtaki au kutaifisha shehena aina hiyo.
Akizungumza na Mwananchi ofisini kwake Darajani
mjini Unguja, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo na Maliasili, Dk
Bakari Asseid, amesema Sheria ya Misitu na Maliasili ya mwaka 1996
haizungumzii rasilimali za misitu zinazokamatwa kutoka nje ya nchi na
kupitia Zanzibar.
Dk Assweid alisema wizara yake imepewa uwezo wa
kukamata mzigo wa aina hiyo na kuurejesha mahali ulikotoka lakini haina
uwezo wa kuwakamata wahusika na kuwafungulia mashtaka mahakamani.
Alisema sheria ya kimataifa ya kulinda misitu na
wanyamapori, walioko katika hatari ya kutoweka imeridhiwa na kusainiwa
na Tanzania, lakini ikiwa haijaridhiwa na Zanzibar.
Pia alisema mambo ya kilimo na maliasili hayamo
katika orodha ya mambo ya Muungano kwamba maazimio na sheria za
kimataifa zinazopitishwa hazijawa na mamlaka ya kufanyakazi Zanzibar.
“Mamlaka ya dhamana tumeshazipa maelekezo ya
kutosha kwa mujibu wa sheria, magogo hayo yanapaswa kurejesha wa mahali
yanakotoka mara moja, hatuna sheria ya kuwashtaki au kutaifisha mzigo
huo, suala hilo liko nje ya uwezo wetu kisheria,” alisema Dk Asseid.
Pia alikiri kuwa Bandari ya Malindi kuanzia Desemba mwaka jana, imekuwa ikisafirisha kiwango kikubwa cha shehena ya magogo.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399
0 comments:
Post a Comment