.Wasimamizi wa Uchaguzi na waangalizi wa vyama
vya siasa wamesema, zoezi la uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki
limekwenda vizuri licha ya kasoro iliojitokeza ya baadhi ya watu kutoona
majina yao katika orodha ya matangazo ya wapiga kura yaliyobandikwa
katika vituo siku 21 kabla ya kufanyika kwa uchaguzi huo.
Wakizungumza na Mwananchi wasimamizi
hao,waangalizi wa ndani walisema vituo vilifunguliwa kwa wakati,vifaa
vilifika mapema na hadi mchana hakukuwa na malalamiko yoyote katika
zoezi hilo la upigaji kura linaloendelea.
Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Uchaguzi
Kiembesamaki, Suluhu Ali Rashid amesema,hadi mchana zoezi la upigaji
kura lilikuwa likiendelea vyema na hakukuwa na malalamiko ya watu
kunyimwa haki ya kupiga kura kidemokrasia katika vituo vya uchaguzi.
Suluhu amesema, amepokea lalamiko moja la maneno
kutoka kwa Mgombea wa Cuf, Abdulmalik Haji Jecha kuwa mawakala wake
hawaridhiki na ukaguzi unaotumika kabla ya kupiga kura kama sheria
inavyoelekeza, wakitaka shahada ya mpiga kura ikaguliwe na mawakala wa
vyama kabla ya kuruhusiwa badala ya kutangaza jina na kuangaliwa katika
daftari la wapiga kura.
Alisema kwa mujibu wa sheria ya Tume ya Uchaguzi
jina la mpiga kura linatakiwa kutangazwa na ofisa wa kituo na mawakala
wa vyama kuangalia jina na picha yake katika orodha ya wapiga kura na si
vinginevyo.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment