Zanzibar
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imeombwa kuipatia fedha Wizara
ya Kilimo na Maliasili kwa ajili ya kulipa deni wanazodaiwa na wakulima
wa mpunga.
Akiwasilisha
ripoti ya Kamati ya Fedha Biashara na Kilimo, Mwenyikiti wa Kamati
hiyo, Salmin Awadh Salmin alisema wizara hiyo inadaiwa Sh milioni 240 na
wakulima.
Alisema
wakulima hao wanadai fedha hizo zaidi ya miezi minne, hali
inayosababisha kurudisha nyuma maendeleo ya kilimo hicho na kukosa
kujikimu kimaisha.
"Kamati
ilielezwa kuwa wakulima wa mikataba wanaozalisha mbegu za mpunga katika
mabonde mbalimbali wanaidai Wizara jumla ya Sh milioni 240 baada ya
Wizara kuchukua mpunga huo bila ya kuwalipa kwa zaidi ya miezi minne
ambapo wakulima wa bonde la Mtwango pekee wanadai Sh milioni 60,"
alisema.
Alisema
tatizo hilo linaweza kuathiri uzalishaji wa mbegu hizo za mpunga,
kitendo ambacho kinawavunja moyo wakulima na kuathiri kilimo hicho.
Salmin
ametaka wizara hiyo ya Kilimo na Maliasili kupatia Chuo cha Kilimo
kilichoko Kizimbani, mtaalam wa maabara ya mifugo na ulinzi wa uhakika
ili kiweze kufanya
Chanzo;habari Leo
0 comments:
Post a Comment