Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein
akipokea zawadi mara alipowasili katika Chuo cha Mafunzo ya Amali
kiitwacho Tilonia, Wilaya ya Ajmer Jimbo la Rajastan akiwa katika siku
ya pili ya ziara yake nchni India pamoja na ujumbe aliofuatana nao.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo na Maliasili Affani Othman Maalim
(kulia) kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar akitiliana saini
makubaliano ya uanzishwaji wa Chuo cha Mafunzo ya Amali kwa Wanawake na
Chuo cha Barefoot cha India ambapo muanzilishi wa Chuo hicho Bw. Bunker
Roy alitia saini (kulia). Saini hiyo ilifanyika wakati Rais wa Zanzibar
na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwa katika
ziara rasmi nchini India na ujumbe wake.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo na Maliasili Affani Othman Maalim
(kulia) akibadilishana hati za makubaliano na Bw. Bunker Roy baada ya
kutiliana saini makubaliano ya uanzishwaji wa Chuo cha Mafunzo ya Amali
kwa Wanawake baina ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Chuo cha
Barefoot cha India, saini hiyo ilifanyika wakati Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akiwa katika
ziara rasmi nchini India na ujumbe wake.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed
Shein akibadilishana mawazo na Bw. Bunker Roy Muanzilishi wa Chuo cha
Mafunzo ya Amali kwa Wanawake katika Kijiji cha Tilonia Wilaya ya Ajmer
Jimbo la Rajastan pamoja na Balozi wa India nchini Tanzania Debnath
Shaw (kulia) baada ya saini ya makubaliano ya uanzishwaji wa chuo kama
hicho Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akiagana na Bw. Bunker Roy.
[Picha na Ramadhan Othamn, Ikulu]
0 comments:
Post a Comment