Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Jaji mstaafu,Joseph Warioba
Kirigini ambaye pia aliwahi kuwa mbunge wa Musoma Mjini kwa miaka 10 mfululizo kuanzia mwaka 1975 hadi 1985, alitoa ushauri huo jijini Dar es Salaam mbele ya waandishi wa habari kuhusu maoni yake katika mchakato wa Katiba, Bunge Maalum la Katiba, Tume ya Mabadiliko ya Katiba, waasisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na matatizo ya rushwa kwenye chaguzi nchini.
“Namuomba Rais Kikwete, alinde heshima ya Warioba na timu yake kwani ndiye aliyewateua kwa ajili ya kukusanya maoni ya mchakato wa kupatikana Katiba mpya, alipokea kazi yao na kuipongeza,” alisema Kirigini na kuongeza:
“Tume ilikuwa na watu wakubwa wenye heshima kubwa, walifanya kazi ya heshima ndani ya miezi 18 kuzunguka nchi nzima kukusanya maoni ya wananchi, lakini leo watu wanamkejeli Warioba.
Vyama vinavyofanya hivyo vinapaswa kukemewa kwani wanafanya ujanja wa kubadilisha maoni ya wananchi.”
Alimuomba Rais Kikwete kutokuwa na kigugumizi anapoona wajumbe wa Bunge la Katiba kutoka vyama vya siasa wanatoa maneno ya kejeli na mipasho huku wakizima midomo ya wajumbe wengine wa bunge hilo kutoka asasi mbalimbali za kiraia.
Kirigini alisema anawaunga mkono baadhi ya wajumbe waliosusia vikao vya mkutano huo wa awamu ya kwanza ya kujadili Rasimu ya Katiba kwa madai ya kwamba waliona wanajadili kitu ambacho hakihusiani na maoni ya wananchi yaliyomo kwenye rasimu hiyo.
Kirigini ambaye ni mwanachama wa CCM alisema aliamua kutoa maoni hayo baada ya kuona mchakato wa Katiba mpya ambao kwa sasa upo katika Bunge Maalumu umehodhiwa na baadhi ya vyama vya siasa.
SOURCE:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment