Home » » Zanzibar yadaiwa Sh. bilioni 294.90

Zanzibar yadaiwa Sh. bilioni 294.90

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Waziri wa Fedha wa Zanzibar,Omar Yussuf Mzee.
 
Waziri wa Fedha wa Zanzibar, Omar Yussuf Mzee, jana alitangaza bajeti ya Zanzibar kwa mwaka wa fedha 2014/15 na kusema serikali mpaka kufikia mwezi wa Machi 2014, inadaiwa Sh. bilioni 294.90 sawa na ongezeko la asilimia 17.0.
Alisema deni hilo limeongezeka ikilinganishwa na deni la Sh. bilioni 252.3 lililokuwapo Machi 2013.

Alisema ukuaji huo umetokana na kutolewa fedha kwa ajili ya miradi inayoendelea kama vile ya ujenzi wa njia ya ndege kuruka na maegesho ya ndege, miradi ya maji safi na salama na miradi ya barabara.

Alisema Kati ya deni hilo, Sh. bilioni 211.8 deni la nje linalomaanisha ongezeko la asilimia 4.0 ikilinganishwa na Sh. bilioni 203.8 kwa Machi 2013.

Asilimia 88 ya deni la nje imedhaminiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano na asilimia 12 Serikali ya Zanzibar na kuwa hadi Machi 2014, deni la ndani nalo liliongezeka hadi Sh. bilioni 83.09.

Hali hiyo imetokana na kuongezeka kwa mikopo kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BoT), deni la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (ZSSF) na deni la wastaafu. Mwaka 2014/15 serikali inatarajia kukusanya Sh. bilioni 707.8  kulinganisha na Sh. bilioni 658.5 za 2013/14.
 
SOURCE: NIPASHE

0 comments:

Post a Comment

 
Support by Blogs za Mikoa Tanzania
Copyright © 2012. Zanzibar Yetu - All Rights Reserved
Designed by by Blogs za Miikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa