Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Makamu wa Kwanza wa Raisi Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad.
Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar, Shaka Hamdu Shaka, alisema ikiwa serikali ya SUK itavunjia wakati wowote,mwanasiasa anyestahili kubebeshwa lawama ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif hamad, kwa kuwa ndiye anaeidhoofisha SUK kutokana na matendo yake.
“Makamu wa Kwanza wa RaIsi Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad ndiye anayeiyumbisha Zanzibar na ikiwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa itavunjika asitafutwe mchawi, ”alisema Shaka katika mkutano wa hadhara. Alisema siri za Serikali zinavuja zimekuwa vikivuja na kujulikana katika makao makuu ya CUF kutokana na Maalim Seif kutokuwa mwaminifu.
Shaka alisema pamoja na kuundwa SUK, lakini bado Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar anasahau mtafaruku wa kisiasa uliokuwapo Zanzibar kabla ya maridhiano.
Akizungumzia msimamo wa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kutaka kuwasilisa hoja binafsi katika kikao kijacho na wananchi kuulizwa kupitia kura ya maoni kama wanaafiki SUK iendelee au la, Shaka alisema hoja binafsi hupelekwa na mwakilishi baada ya kuijengea nguvu ya hoja na si ya chama cha siasa hivyo anayetaka kufanya hivyo ana haki isiyozuilika.
Alisema hata hoja iliyopendekeza SUK haikuwasilishwa barazani na CUF au CCM bali ilipelekwa na mwakilishi wa Mgogoni, Aboubakary Khamis Bakary wa CUF kama Mwakilishi Salmin Awadh Salmin wa CCM jimbo la Magomeni atakavyoipeleka kwenye chombo hicho ikisubiri maamuzi kupitia kura ya maoni.
Maalim seif alipotafutwa jana kuzungumaia madai hayo hakupatikana.
SOURCE:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment