Home » » SMZ YAFUTA VAT KWA VIFAA VYA UUEME

SMZ YAFUTA VAT KWA VIFAA VYA UUEME

 SEIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imefuta kodi ya ongezeko la thamani (VAT), kwa vifaa vya umeme vya matumizi ya nyumbani yakiwamo majiko ya gesi, kwa lengo la kupunguza matumizi makubwa ya umeme visiwani Zanzibar.

Uamuzi huo ulitangazwa jana na Waziri wa Maji, Ujenzi, Nishati na Ardhi, Mansour Yusuf Himid, alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Shangani, mjni Zanzibar.

Alisema majiko yote yanayotumia gesi hivi sasa yataingizwa Zanzibar bila kutozwa VAT, ili kuwawezesha wananchi wengi kumudu gharama zake kwa vile ni hatua moja itakayosaidia kupungaza matumizi makubwa ya umeme.

Serikali imeamua kuchukua hatua hiyo ili wananchi wengi waweze kutumia nishati ya gesi kwa matumizi ya nyumbani, hatua itakayosaidia kupunguza uharibifu wa mazingira na kuwapuguzia makali ya maisha wananchi.

“Tumeamua kufuta kodi ya VAT ya asilimia 20 kwa vifaa vya umeme wa matumizi ya nyumbani, zikiwamo balbu zinazotumia umeme mdogo, majiko ya gesi, vifaa vya umeme wa jua na umeme unaotumia upepo,” alisema Mansour.

Serikali imelazimika kuchukuliwa hatua hiyo, ili wananchi wengi waweze kunufaika na umeme ambao umeanza kupatikana Zanzibar, unaozalishwa kwa mionzi ya jua, hivyo kuwanufaisha na wananchi wengi wakiwemo wa vijijini.

Wananchi 12,000 wa kisiwa cha Tumbatu wataanza kupata huduma ya umeme baada ya mradi wa kupeleka umeme kukamilika mwishoni mwa mwaka 2009.

Gharama za kukiunganisha kisiwa hicho cha Tumbatu inatarajia kuwa sh milioni 800. Kazi ya kutangaza zabuni inatarajiwa kufanywa na Kampuni ya NorPlan kabla ya kuanza utekelezaji wa mradi huo.

Alieleza fedha za kuunganisha umeme katika kisiwa hicho zimepungua kutoka sh bilioni 1.6 hadi sh milioni 800 kutokana na kupungua kwa gharama za mafuta na madini ya shaba ambayo yatatumika katika kutengeneza waya maalum utakaotandikwa chini ya bahari.

Kisiwa cha tumbatu kinakabiliwa na ukosefu wa umeme na kuathiri harakati za kiuchumi kwa wananchi wake ambao hutegemea shughuli za kilimo na uvuvi.

Chanzo;Tanzania Daima
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

Post a Comment

 
Support by Blogs za Mikoa Tanzania
Copyright © 2012. Zanzibar Yetu - All Rights Reserved
Designed by by Blogs za Miikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa